STREET SMART
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 832
- 660
Wanajamii naomba mnisadie ushauri wa kisheria, Marehemu baba yangu alikuwa anamiliki eneo lenye nyumba na mabanda ya biashara, lenye Certificate of Ocupancy ya mwaka 1980 na kibali cha kuendeleza ujenzi kilichotolewa na afisa ardhi wa wilaya mwaka 2007, eneo lipo wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara.
Sasa juzi tumepokea barua ikitutaka kuvunja kila kitu kilichopo umbali wa mita 22 kutoka barabarani bila ya kufidiwa chochote. Ningependa nijue sheria inasemaje juu ya hili swala na naweza kuchukua hatua gani za kisheria kuanzia sasa.