Hi lady N.
Uimara sio wa brand tu bali model. Japo generally kuna brand nyingine kama dell zinasifika lakini kuna
model fulani fulani za brand hizo zinaweza kuwa zina design defect. Baadhi ya model za Hp na Dell ukisoma
reviews za watumiaji kadhaa zina matatizo ya power supply kwenye ubao mama( Mother board) na hivo kusababaisha laptop kujizima zima .
Hiyo haimaanishi samsung kuwa ni imara.
Kwa hiyo ushauri wangu wa awali
- Tambua kwanza model ya kila aina ya brand ulizoona au ulizopenda au zene bei unayoweza. Mfano HP NX9600 Dell Insipiron
- Soma review za kila model kutoka kwa wadau mbalimbali mtandaoni.Au weka majina ya model zako tukuwekee copy and paste au link ya reviews za wadau mbali mbali
- Fanya maamuzi.
NB
Kwa haraka haraka kama
uimara ni kigezo cha muhimu sana ukiondoa
Dell uliyoweka Jaribu kudodosa na model za
Toshiba.
Vile vile
Matumizi ya laptop yanaweza yakaongeza au yakapunguza uimara wa kitu kulingana na specs zake.
Kama ni kwa ajili ya matumizi ya shule na mtumiaji ni mtu mmoja nahakika laptop yeyote utakayochukua katika hizo itakuwa imara . Assuming zote zitakuwa zina processing capacity sawa sawa.
Lady N tunaweza kufanya doorshopping tena na mtazamaji kama uko tayari. Hiyo ni volunteeer tena kwako tu.