msaada plz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada plz

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Lady N, Oct 9, 2012.

 1. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mie kwenye haya mambo ya teknolojia si mzoefu sana, nataka kununua hivi vilaptop vidogodogo, ktk window shopping niliona hp, dell na sumsung (2gb ram na 320gb hard disk kwa zote), ktk hiz ipi ni imara? ukinipa na sababu itakuwa vizuri pia (kwa level yangu ya IT specification naishia hapo, kama waweza kunipa specification nyingine muhim za kucheck kabla ya kununua pia itakuwa bomba)
   
 2. N

  Nyasiro Verified User

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 1,286
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  umesahau processor speed ni muhimu sana
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hi lady N.

  Uimara sio wa brand tu bali model. Japo generally kuna brand nyingine kama dell zinasifika lakini kuna model fulani fulani za brand hizo zinaweza kuwa zina design defect. Baadhi ya model za Hp na Dell ukisoma reviews za watumiaji kadhaa zina matatizo ya power supply kwenye ubao mama( Mother board) na hivo kusababaisha laptop kujizima zima .

  Hiyo haimaanishi samsung kuwa ni imara.

  Kwa hiyo ushauri wangu wa awali
  1. Tambua kwanza model ya kila aina ya brand ulizoona au ulizopenda au zene bei unayoweza. Mfano HP NX9600 Dell Insipiron
  2. Soma review za kila model kutoka kwa wadau mbalimbali mtandaoni.Au weka majina ya model zako tukuwekee copy and paste au link ya reviews za wadau mbali mbali
  3. Fanya maamuzi.


  NB
  Kwa haraka haraka kama uimara ni kigezo cha muhimu sana ukiondoa Dell uliyoweka Jaribu kudodosa na model za Toshiba.

  Vile vile Matumizi ya laptop yanaweza yakaongeza au yakapunguza uimara wa kitu kulingana na specs zake.

  Kama ni kwa ajili ya matumizi ya shule na mtumiaji ni mtu mmoja nahakika laptop yeyote utakayochukua katika hizo itakuwa imara . Assuming zote zitakuwa zina processing capacity sawa sawa.

  Lady N tunaweza kufanya doorshopping tena na mtazamaji kama uko tayari. Hiyo ni volunteeer tena kwako tu.
   
 4. Fatma Bawazir

  Fatma Bawazir JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  na kingine cha kuongezea usichukue laptop ambazo zina pumulia kwa chini au feni yake ya kupoza isiwe inavuta hewa kwa chini maranyingi toshiba ana feni yake inapumulia kwa pembeni na haipati moto na hainyonyi vumbi kirahisi hizo ni toshiba na dell na huo ndio chanzo kikubwa cha ugonjwa kwa laptop unakuta laptop inapumulia kwa chini halafu mtu anaiweka juu ya kitanda au kochi kwa muda mrefu
   
 5. leh

  leh JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mkuu kama upo Dar unijulishe nikirudi nikununulie soda, kama upo atown, ndo uniambie siku ya leo. kila siku najaribu kuwaeleza watu wa hapa jamvii kuwa hamna brand inazidi brand nyingine lakini wap. nafurahia kuona una uelewa kama mimi
  :focus:

  Lady N
  kama mkuu hapo juu alivyosema, huwezi decide kuwa ni laptop za brand ipi ni bora kuliko zingine, ila model zao zinatofautiana. kila mtu hapa jamvi forums atakupa jibu tofauti, mfano mi hapa napendelea mini laptop iwe ya Samsung au Acer Aspire, haswa za Acer because wao ndo wana mini laptops zinazohifadhi moto mno zikifuatiliwa ni za Samsung Atom. ila hii si kumaanisha kuwa mini laptop za Samsung au za Acer ndo bora. the best way kujua ni laptop ipi bora kuliko nyingine ni kwanza na specification zake ila we umesema sio mtaalamu wa IT, my advice would be to either (a) uwe na mtaalamu zaidi kama Mtazamaji alivyo volunteer au (b) uchague laptop kama tatu ulizopenda dukani ukaomba wakupe model zake upost hapa jamvii, watalam wengi na kukusaidia tutakusaidia
  leh
  [​IMG]
   
 6. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,766
  Likes Received: 7,070
  Trophy Points: 280
  Good to see you back mkuu nilimiss lecture kama hizi siku nyingi
   
 7. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  nawashukuru wote kwa michango yenu, ni ya muhimu sana kwangu na nitaifanyia kazi.
   
 8. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280

  Mkuu kama nimemuelewa vizuri mtoa mada amesema mini laptop! Hivi Dell,Toshiba na HP wameshatoa mini laptops kweli?

  Kwa uelewa wangu mfupi makampuni yanayoongoza sokoni kwa kutoa aina hiyo ya laptop ni ASUS,ACER na SAMSUNG!

  Mchango wangu: Ndugu mtoa mada kwa experience yangu kiduchu nimetokea kuiamini sana mini laptop ya ASUS kwanza kwa uwezo wake wa kuhifadhi chaji na kutokuwa na usumbufu/matatizo ya mara kwa mara. Nina mwaka wa 3 sasa naitumia mini laptop ya ASUS na sijawahi kuface tatizo lolote kubwa la kiufundi! Binafsi napendekeza ASUS!
   
 9. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,287
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  hii nilikuwa siifaham sana thenkyu kwa kutujuza, ninayo laptop ya GATEWAY haipati moto kabisa unaweza iweka kwenye mapaja hata saa moja ukafanya shughuli zako ukamaliza, lakini nina mdogo wangu anayo dell inapata moto hiyo utafikiri jiko!
   
 10. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kuna mambo mengi sana nilikuwa siyajui na najifunza kupitia hapa, thumb up for u all
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu Unaweza kuwa sahihi lakini unaona na wewe mwenyewe unasema huna uhaika kama dell na HP wana Mini laptop lakini mleta mada anasema katika "dirisha la mununuzi"( Windows shopping )alilofanya aliona/ alipenda Dell, HP na samsung . Je zote hizo zilikuwa min laptop?

  Nadhani way foward atuelezee hizo model ya hizo brand then tutajua kama anahitaji laptop au mini.
  Btn kwa maendeleo ya teknoljia sasa hivi kuliko kununua mini laptop bora ununue tablet za (samsung/ hp , asus etc ) au ipad. Ingaw sijajua ema mahitaji yake na matumizi yake mi namshauri anunue Laptop au Tablet.


  wakati tunaendelea n mjadala naomba utupe taarifa zaidi zinazoweza kumsaidia mleta mada . Unaweza kutumbia hiyo mini laptop ya asus ni model gani na kuikamata unatakiwa uwe na kadiriao la laki ngapi?


  Teh teh teh leh Mkuuu leh Aksante sana. Katika dunia hii ya TEHAMA location ya mtu haitakwii kuwa kikwazo. Hiyo soda nirushie tu kwenye MPesa,Tigopesa au Airtelmoney..... Tupo pamoja
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...