msaada plz nimechoka kukaa kwa ndugu

msaada plz nimechoka kukaa kwa ndugu

JASX

Senior Member
Joined
Aug 26, 2012
Posts
170
Reaction score
130
Habari ya jioni wana jf. Naomba ushauri. Naishi kwa uncle ambaye ni kama baba yangu kanisomesha toka primary mpaka chuo first year namshukuru kwa hilo sana. Nimeishi nae kutoka 2006 mpaka sasa miezi ya likizo. Uncle hana tatizo lakini kuanzia shangazi, ndugu yake shangazi na wasichana wake wa kazi wamenifanya nichoke kabisa kuishi pale. Nimemwambia uncle kuwa maisha ya pale kwake yamenishinda nataka nikaishi sehemu nyingine tofauti na pale. Kanijibu mtoto wa kike haachi wazazi wake na kupanga pia dharau.
 
anko mbna ana mambo ya kizaman ? Km vp njoo kwangu upunguze stress
 
Una kipato gani we mtoto wa kike kitachokuwezesha kujitegemea katika kuendesha hayo maisha ya kupanga?

Au unadhani kupanga hapa jijini ni rahisi!!
Usijitafutie shida na kuanza kutembea usiku kucha mitaani. Muda bado endelea kulelewa na mjomba.
 
Ndugu vumilia hakuna lisilokuwa na mwisho, jifunze kutokujali chochote watakachokufanyia kisikuumize kichwa wao wenyewe watachemka na punguza muda wa kukaa home kama uko chuo tumia muda mwingi kuwws chuo

Nakubaliana na wewe, huyu binti kama alivumilia tangu primary mpaka first year chuo, unashindwa nini kuvumilia kwa miaka miwili au mitatu iliyobaki? Kwa nini asitafute room hostel kama nyumani hakukaliki? \inawezekana kabisa nyumbani kwao pamekuwa pagumu lakini pia inawezekana anatafuta moral support ya kwenda kuishi sehemu anayoiona ina uhuru zaidi wa kufanya mambo yake yasiyo ya kishule. Ni bora avumilie na kukaza kwenye masomo au kama mambo ni magumu zaidi amwombe mjomba wake amtafutie hostel.

Haya mambo ya kupanga chumba kwa mtoto wa kike tena wa first year, kuna madhara makubwa na hasa mjomba atakapokasirishwa na kitendo cha kuhama nyumbani na kuamua kusitisha huduma, anaweza kuishia kujiuza.
 
Mtakuwa pia mnashindwana kwenye kazi za nyumbani.....najua mara nyingi ndipo chokochoko zinapoanziaga hapo.
 
Anataka aishi kama yuko hotelini.
Kama aliweza kuvumilia miaka yote hiyo anashindwaje sasa wakati soon atamaliza chuo? JASX street maisha sio rahisi kama unavyofikiri,hala hala usinyee kambi tu.
 
Last edited by a moderator:
Siko mbali sana na wadau wengine naona ni vema ukaendelea kukaa hapo kwa mjomba wako. Kama umekaa hapo kwa muda huu wote jiulize kwanini wamebadilika , pengine wewe mwenyewe umechange. Kosa ulilofanya ni hapo ulipomwambia uncle wako kua hapo home pamekushinda hii si lugha nzuri. Ungetaka mjomba wako akubaliane na wewe kwamba mkewe ana tatizo wakati umekaa nao muda huo wote? Kumbuka uvumilivu siku zote unalipa na si vizuri hata kidogo kuwalaumu unaoishi nao hata kama wanakunyanyasa, wewe ni kijana/binti mkubwa sasa . Kumbuka hao si wazazi wako hivyo yakupasa uwavumilie na ujaribu wakati wote kuongea kwa busara na mjomba wako. Hata akiona umenyanyaswa na akakuuliza unaonaje maisha ya nyumbani we sema mazuri tu tena namshuru sana shangazi amekua msaada sana kwangu. Tumia muda wako mwingi chuoni au kwa marafiki zako na bila kusahau kushirikiana na hao wadada wa kazi uwapo home. Kumbuka mtaka cha uvunguni sharti ainame
 
mleta mada: huyo 'boiflend' atakuruka mita 100 ukidaka mimba. we jaribu uone.
 
Anataka aishi kama yuko hotelini.
Kama aliweza kuvumilia miaka yote hiyo anashindwaje sasa wakati soon atamaliza chuo? JASX street maisha sio rahisi kama unavyofikiri,hala hala usinyee kambi tu.

Ni ngumu kuishi na watu kama sio mvumilivu ma d......alipotoka ni mbali lakin anapokwenda nikaribu sana.
Jitume mamito,najua kusoma kunahitaji muda sana lakin kazi za nyumbani usikose.....sio kisa unasoma hata kuosha kikombe bas unasingizia assignment.
NB;kupanga si lele mama dogo,ingawa yawezekana visharo vimeanza kukuzengea.....wanakupenda kwakuwa upo kwa uncle ila ukitoka hapo hawana ubavu wakukuhudumia zaid wakujaze mimba basiiii!!!!
 
Hapo kwa red umelenga mule mule,mtu anaweza ashinde amelala akiamka dining akimaliza assignment.
Haijulikani weekdays,weekends wala likizo hakuna siku yuko available its either amechoka au yuko busy.
 
Kama umeshinda nyumba ya airtel hamia vinginevyo endelea kubaki kwa mjomba kitu chochote kigumu unachokumbana nacho ktk maisha chukulia kama changamoto maana hapo ndo pa kujifunzia leo ukisema uondoke huko uendako ukikutana na same changamoto utahama Au?
 
Mtakuwa pia mnashindwana kwenye kazi za nyumbani.....najua mara nyingi ndipo chokochoko zinapoanziaga hapo.
Nahisi pia kuna kawivu hapo anaonekana binti yuko vizuri hadi kafika chuo, hatujui hao wandugu wana-perform vipi masomoni !!!!
 
Habari ya jioni wana jf. Naomba ushauri. Naishi kwa uncle ambaye ni kama baba yangu kanisomesha toka primary mpaka chuo first year namshukuru kwa hilo sana. Nimeishi nae kutoka 2006 mpaka sasa miezi ya likizo. Uncle hana tatizo lakini kuanzia shangazi, ndugu yake shangazi na wasichana wake wa kazi wamenifanya nichoke kabisa kuishi pale. Nimemwambia uncle kuwa maisha ya pale kwake yamenishinda nataka nikaishi sehemu nyingine tofauti na pale. Kanijibu mtoto wa kike haachi wazazi wake na kupanga pia dharau.
Kama unahisi utaweza kujilipia pango basi mwambie uncle kwamba shule ya mwaka wa pili ni tafu balaa bila ya kukaa hostel basi mambo yatakua magumu, lakini ukisema umshirikishe katika hela ya pango hapo mtashindwana bureee!!!!
 
Habari ya jioni wana jf. Naomba ushauri. Naishi kwa uncle ambaye ni kama baba yangu kanisomesha toka primary mpaka chuo first year namshukuru kwa hilo sana. Nimeishi nae kutoka 2006 mpaka sasa miezi ya likizo. Uncle hana tatizo lakini kuanzia shangazi, ndugu yake shangazi na wasichana wake wa kazi wamenifanya nichoke kabisa kuishi pale. Nimemwambia uncle kuwa maisha ya pale kwake yamenishinda nataka nikaishi sehemu nyingine tofauti na pale. Kanijibu mtoto wa kike haachi wazazi wake na kupanga pia dharau.

kwa mujibu wa maelezo yako nnashawishika kukuuliza una miaka mingapi?
maana tabia ulizo nazo ni za binti anaeanza kupitia foolish age, umekaa na uncle wako kwa mda wote huo hakukua na tatizo ila tatizo limeanza baada ya kwenda chuo??
katika umri wako vijana wengi tabia hubadilika, hata ungekaa kwenu tofauti ingekuwepo tuu, ungeweza kuwalaumu pia,
kikubwa nikushauri ubadili tabia yako na iwe kama zamani, epuka makundi yasiyofaa na jitahidi kuwa kwenye ibada na masomo usiyaweke kando
 
Nahisi pia kuna kawivu hapo anaonekana binti yuko vizuri hadi kafika chuo, hatujui hao wandugu wana-perform vipi masomoni !!!!

Hutokea wivu lakin binadamu unatakiwa uishi nae kwa akil sana......ukipanga ratiba yako vizur na ujishughulishe na shughul za nyumbani wataishia poroji tu hapo ndo pakuwabaini.
 
Habari ya jioni wana jf. Naomba ushauri. Naishi kwa uncle ambaye ni kama baba yangu kanisomesha toka primary mpaka chuo first year namshukuru kwa hilo sana. Nimeishi nae kutoka 2006 mpaka sasa miezi ya likizo. Uncle hana tatizo lakini kuanzia shangazi, ndugu yake shangazi na wasichana wake wa kazi wamenifanya nichoke kabisa kuishi pale. Nimemwambia uncle kuwa maisha ya pale kwake yamenishinda nataka nikaishi sehemu nyingine tofauti na pale. Kanijibu mtoto wa kike haachi wazazi wake na kupanga pia dharau.

Haha huna mtu? chukua kitumbo then hamia kwa jamaa jumla jumla. kama huwezi basi vumilia
 
Back
Top Bottom