Msaada please ndoa ya kanisani (Roman Catholic)

Msaada please ndoa ya kanisani (Roman Catholic)

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,755
Reaction score
2,303
Habari wana jukwaa, Naomba kuuliza tu kwa wanaoifahamu vizuri taratibu ya kufunga ndoa ya kanisa Catholic. (RC)

Ndugu yangu anataka na ndoto yake ni kufunga ndoa ya kanisa Catholic, Lakini hajabatizwa wala hakuwa muumini wa kanisa hilo hapo mwanzo Japo analipenda, Lakini inasemekana kwamba kanisa Catholic lina masharti mengi kwenye utaratibu wa kufunga ndoa na ubatizo. Je ni kweli?

Please kwa wanaojua nini cha kufanya ili atimize adhima yake na kuwa muumini wa kanisa hilo?. Anataka kufunga ndoa mapema mwakani.

Mwongozo kwa wanaojua.
 
Mchumba wake ni Mkatoliki?

Akionana na Paroko anaweza anza mafundisho na kupata sakrament zote siku moja. Yaani Ubatizo, Communio, Kipaimara na Ndoa.
 
Kwa Daslamu..Kama hajabatizwa anapaswa abatizwe kwanza,atapewa na sacrament zingine, then ataenda mafundisho kwa miezi sita, atapigwa Pepa, akifaulu ndo ataruhusiwa kuanza taratibu za ndoa.
 
Mchumba wake ni Mkatoliki?

Akionana na Paroko anaweza anza mafundisho na kupata sakrament zote siku moja. Yaani Ubatizo, Communio, Kipaimara na Ndoa.
Asante sana mkuu mchumba nae sio mkatoric pia!
 
Kwa Daslamu..Kama hajabatizwa anapaswa abatizwe kwanza,atapewa na sacrament zingine, then ataenda mafundisho kwa miezi sita, atapigwa Pepa, akifaulu ndo ataruhusiwa kuanza taratibu za ndoa.
Duuh pepa tena, any way sawa mkuu asante kwa mwongozo
 
Kama NI wewe nakupa hongera kwa kuamua kuchagua kufunga ndoa katika kanisa teule takatifu la mitume lililoasisiwa na Yesu Kristo mwenyewe na kupuliziwa pumzi ya Roho mtakatifu wa Mungu. Bali Kama sio wewe basi nifikishie pongezi hizi kwa muhusika.

Tumsifu Yesu Kristu (Laudetur Iesus Kristus). Iwapo muhusika/wahusika hawakubatizwa ubatizo wa maji na roho (katoliki pia inatambua ubatizo wa madhehebu ya Anglikana na Lutheran) basi itawapasa kwanza wabatizwe kwa ibada ya ubatizo itakayowaongoza kumkataa shetani na mambo yake yote na kumkiri Kristo kwamba ndiye Bwana na mwokozi wao, chini ya usimamizi na maongozi ya baba/mama wa ubatizo.

Baada ya hapo watapatiwa mafunzo kea ajili ya kupata sakrament nyingine mbili ambazo NI katekumeni (komunio ya kwanza) na kipaimara. Kuna wakati hizi sakramenti zote tatu zinaweza kutolewa kwa wkati mmoja Kulingana na jinsi mtu alivyoiva na Mara nyingi inakukuwa wakati wa misa za mikesha ya Krismass au pasaka depending na availability ya askofu wa Jimbo kwa sababu sakramenti Kama ya kipaimara ni lazima itolewe na askofu mwenyewe.

Mkisha maliza hizo sakramenti tatu muhimu mtaanza Sasa mchakato wa kupata mafunzo ya ndoa baada ya kutimizo vigezo vyote vya usajili ikiwemo kuandikisha ndoa parokiani unakoishi na tangazo lako la ndoa litasomwa kwa wiki tatu mfulizo kwenye parokia uliyojiandikisha, parokia ulikozaliwa na parokiani kwa mwenza wako alikozaliwa ili endapo Kuna pingamizi lolote basi liweze kuwasilishwa. Lakini pia utapaswa kulipia malimbikizo ya zaka na na fungu la kumi, (hapa Mara nyingi paroko anakukadiria Kulingana na utakavowasilisha kipato chako Cha mwaka au mwezi). Wakati huo unakuwa unaendelea na mafundisho ya ndo yanayochukua miezi mitatu (sio kila siku inaweza kuwa Mara moja au mbili kwa wiki na yanatolewa na walimu, makatekista na mapadiri wazoefu).

Mkishamaliza mafundisho ya ndoa Sasa mtakuwa tayari kufunga ndoa halali na takatifu yenye upako wa Roho Mtakatifu mwenyewe katika tarehe na kanisa ambalo mme lichagua. Mimi nilifingia St Joseph Dar miaka michache iliyopita .

Karibu kwenye chama la wanaojitambua mkuu.

Tumsifu Yesu Kristu.

NB: Hakuna short cut katika hilo au Jambo lolote linalosimamiwa na kanisa Katoliki. Ni kufuata utaratibu tuu. Hili sip kanisa la kihuni kwani Lina pumzi ya Mungu ndani yake.
 
Wewe nenda kanisani hapo utapewa utaratibu nini chakufanya hakuna cha pesa wala nini utalipa vinavyotakiwa kulipiwa sio ukiwa na pesa zako ile sio kikoba, hujasikia mchungaji Kmaro wa KKKT alikuwa na mwanaye wa kiroho alitaka kuwa padri alimpeleka na sahizi ni padri! Nenda hapo hapo parokiani, hongera sana kwa uamuzi mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom