Msaada nyumba inapovuja

Mponda Mponda

New Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
4
Reaction score
0
Habari zenu ndugu zangu wana JF
Naomba walio na maarifa wanisadie namna ya kuziba nyumba yangu ambayo mabati yanavuja mno. Ni nyumba mpya na nilitumia haya mabati yanayoitwa ya migongo mipana, nilinunua pale Buguruni, cha ajabu baada ya kuezekwa kuna maeneo kadhaa yanavuja. Nashindwa kuezua mabati kwani sina uwezo wa kununua mapya.
Tuliweka dawa iitwayo Maroow katika misumari na baadhi ya maeneo yanayopishana mabati lakini wapi, baadhi yalizibika mengine bado
Tatizo ni kwamba kuna maeneo unakuta maji yanavuja lakini hujui chanzo ni wapi huko juu
Hali ni mbaya je kuna gundi jingine bomba au nifanyeje?
Nisaidieni mwenzenu
 
Nunua gundi ya kuzibia inaitwa 'gasket maker' ipo katika tube ya green.
Mark sehemu zinapovuja hata wewe mwenyewe waweza kuziziba.

Pia inawezekana tatizo ni mbao za 2X4 zilipigwa chache yaani kuna gape kubwa kutoka mbao na mbao.
Hapo anahitajika fundi mzuri wa kurekebisha.

Nilikuwa na tatizo kama hilo but nimeshali'solve kwa njia hizo hapo nilizokuelekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…