Msaada: Nyuki wamevamia nyumbani kwangu

Msaada: Nyuki wamevamia nyumbani kwangu

Udogoni tulikuwa tunatumia moto, sasa hawa wa kwenye paa kuwatimua na moto ni hatari
Mkuu hao nyuki wanaweza kuwa wanapumzika kwa muda tu na baada ya siku moja au mbili wataondoka na kuendelea na safari yao. Hili ni jambo la kawaida sana kwa nyuki wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine hasa wakati wa jua kali. Hivyo fanya uchunguzi kuona kama wamefanya makao au wanapumzika tu. Ni rahisi sana kujua kama wamefanya makao kama kuna kitu kama pango au wameingia ndani ya dari nk. Usikubali kutumia njia za kikatili kama dawa ya rungu au moto kama watu wanavyokushauri. Njia nzuri kama unadhani wamefanya makao ni kuchoma moto kwa chini na ule moshi utawafukuza.
 
6cb86e2e192c46596cc4d5e4cc0e322a.jpg

Hapo kwenye rangi nyeusi nimeshindwa kuwasogelea
Kulingana na hii picha uliyoweka inaoneka wameweka mapumziko ya muda baada ya kusafiri mbali. Muwe waangalifu tu msiwachokoze na baada ya muda watajiondokea na kuendelea na safari yao.
 
Mkuu hao nyuki wanaweza kuwa wanapumzika kwa muda tu na baada ya siku moja au mbili wataondoka na kuendelea na safari yao. Hili ni jambo la kawaida sana kwa nyuki wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine hasa wakati wa jua kali. Hivyo fanya uchunguzi kuona kama wamefanya makao au wanapumzika tu. Ni rahisi sana kujua kama wamefanya makao kama kuna kitu kama pango au wameingia ndani ya dari nk. Usikubali kutumia njia za kikatili kama dawa ya rungu au moto kama watu wanavyokushauri. Njia nzuri kama unadhani wamefanya makao ni kuchoma moto kwa chini na ule moshi utawafukuza.
Naandaa moshi hapa niwafurumue
 
Usije logwa ukasema unamuua hata mmoja wao akikusogelea nyumba zima mtahama na kumbuka nyuki wana uwezo wa kuua.Ukiua mmoja tu utafikiri wanaambiana ila ukweli wanasikia harufu ya mwenzao aliyeuliwa wanajua hatari imeingia malkia anakwenda kuuwawa wana uwezo wa kufukuza watu umbali mrefu sana hata ukiingia ndani ya maji ziwani wanakusubiri juu take care bro
 
Katoe taarifa kituo cha polisi mkuu..
Nyuki si viumbe vya kuchezea, huone watakushauli nini.. Kisheria hata mashamba ya nyuki yanatakiwa kuwa angalau mita mia 400 kutoka makazi ya watu..
Usijaribu kuwafukuza kwa moshi nyuki kama wameweka makazi hapo ujue kuna na malkia wao hivyo nyuki hufanya kila mbinu kumlinda malkia, tegemea fight back ya hatari ukifanya hilo jaribio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalilli ya mafanikio na utapata pesa nyingi Sana.... Kwa mie nilietoka ukoo wa walina asali nisingewafukuza
 
Hauja dhulumu mtu Mali yake mkuu? Maana kuna jamaa alitumiwa nyuki kama hivyo na wataalam. Wenye nyumba walikuwa kazini...dada wa nyumbani akaamua kuwasha moto ili awafukuze. Paa lilishika moto na nyumba yote iliteketea. Baada ya hapo nyuki walitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
 
Wakati nafika nyumbani leo nimekuta NYUKI wamejikusanya kwenye paa la nyumba,

Ni sehemu ya hatari maana kila mtu anapita.

Naomba msaada nitumie njia gani kuwatoa maana nimeona kuwatoa kwa moto haiwezekani.

Au kama kuna dawa ya kuwafukuza naomba msaada. Shukrani

Private geologist
Hata hili ni lakuomba msahada,,upo dar eeh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Washa moto, moshi wake watakimbia.

Tena ukipata bangi ukanyanganya inakuwa rahisi sana.

Ina maana udogoni hukuwa unarina asali au kula asali za mitini porini????????????????????????????
sio kila mtu anatokea Tabora kwenye miti na asali.Mfano mtu wa Kariakoo ukimwambia mambo ya kurina asali hakuelewi.
Wapo watu atu watoto unakuta hajawahi kumuona nyuki toka azaliwe
 
Back
Top Bottom