Mkuu hao nyuki wanaweza kuwa wanapumzika kwa muda tu na baada ya siku moja au mbili wataondoka na kuendelea na safari yao. Hili ni jambo la kawaida sana kwa nyuki wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine hasa wakati wa jua kali. Hivyo fanya uchunguzi kuona kama wamefanya makao au wanapumzika tu. Ni rahisi sana kujua kama wamefanya makao kama kuna kitu kama pango au wameingia ndani ya dari nk. Usikubali kutumia njia za kikatili kama dawa ya rungu au moto kama watu wanavyokushauri. Njia nzuri kama unadhani wamefanya makao ni kuchoma moto kwa chini na ule moshi utawafukuza.