Msaada: Njia rahisi za kupunguza mwili

Unene ni mzigo bro.

Mimi nanenepa tu situmii sana vitu vya sukari, mafuta sio mlaji sana labda kwasababu sifugagi mademu pasua vichwa.

Nagawa nguo zangu kibao kwasababu ya hili li mwili.
Miezi 3 iliyopita nimenunua tshirt , kibao lakini sasahivi zimenibana, hasara tu
 
tumejifunza kazi ya protini ni kijenga mwili, sayansi darasa la 3, mwenzako anataka kuubomoa

Ni kweli, na kwa kutumia protini unaenda kubomoa zile kuta za mafuta zinazojitengeneza kwa kutokana na wanga na sukari.

Ktk mwili kuna process ili chakula kiwe energy, protin process yake ni rahisi kulinganisha na vyakula vya wanga na sukari, hivyo kutokana na malimbikizo(kufuatia tunakula milo mi3 inayohusisha wanga na sukari) wanga inabadilishwa kuwa mafuta ili itunzwe kwa matumizi ya baadae, sasa yale ndo yanyofanya upate kitambi..........

hii ni kama hesabu ya kujimlisha na kutoa.....

Ili kupunguza futa lisilo na ulazima mwilini, unatakiwa kuondoa visababishi vya hilo futa... unapoacha kula wanga na sukari, yale yaliyopo yatatumiaka hadi kufikia kiwango chenye uwiano, hivyo protini itafanya kazi yake kwa ufasaha..... kujenga mwili(kujenga mwili haimaanishi kukupa kitambi, bali kuulinda, kuboresha na kuurepea pale kunapokuwa na uharibifu)
 
Naomba ufafanuzi zaidi!
Kwamba Kwa muda huo unakunya hiyo juisi ya tango peke Yake asubuhi , mchana na jioni? Au Mtu anaweza kula kidogo vyakula vingine?
 
Swala la kupungua uzito linahitaji subra!
Kama unapungua kilo moja moja Mbona si haba ?!
Endelee hivyo hivyo bila kukata tamaa utaweza kufikia malengo yako!
Ukishapungua changamoto nyingine ni jinsi ya ku mainten huo uzito mdogo au wa wastani uutakao!
Ndo maana swala kama hili linatakiwa kubalidilisha mfumo mzima wa maisha !
 
Ushawahi kuangalia mchezo was WWE, ushamuona mtu kama John Cena, marehemu Umaga, Randy orton, Tripple H, Dyane, na wengine wengi, ushaona uwezo wao wa kuruka juu, sarakasi za kila namna, ushajiuliza ni kwann wameweza kufanya vile? Jibu ni kwamba unaweza kuwa na kilo nyingi lkn bado ukawa mwepesi, na unaweza kuwa na kilo chache na bado ukawa mzito. Chagua mazoezi yatayokufanya uwe mwepesi na sio kupunguza kilo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MADHARA YA KITAMBI
ini kuhifadhi sumu na kushindwa kutoa insulin ambayo hupelekea maradhi ya::-
kisukari ambayo hufanya mwili kukosa nguvu za kukabiliana na magonjwa yanayoushambulia mwili ikiwa ni pamoja na
nguvu za kiume, ukiwa na tatzo hili unaweza kushindwa kumuingilia mkeo au kwenda safari moja tu
mwanamke kupata tabu ya kupata ujauzito kwa sababu wanazalisha homini ya androgen ambayo huzuia kupata siku zake pia hufanya mzunguko wa m,mke kusumbua
magonjwa ya mzunguko wa damu ikihusisha moyo pamoja na mishipa yake ambayo hupelekea kupata PRESHA NA KIHARUSI
cjui kwann mwanaume akipungua kitambi dhakari yake huongezeka nchi moja au zaidi

DAWA YA KUPUNGUZA MWILI NA KITAMBI

TAFUTA UNGA WA MJAIDURU KIJIKO KIMOJA CHA CHAI VURUGA KWENYE MAJI YA UVUGU VUGU NA SI YAMOTO KIKOMBE KIMOJA

KUNYWA KAMA HIVYO KUTWA MARA TATU UJE UNIPE JIBU BAADA YA CKU 21
KWA USHAURI NA TIBA WASILIANA NAMI AU DR MWINYI
WENU KATIKATI TIBA ASILIA
SULAYMAN
0655821550
hivi nauliza mkuu huu mjaiduru ni mti gani kiengereza tafazari
 
Nilifikisha kilo 90 na mimi ni 5.6” tu. Nilianza kupata matatizo ya high BP.
Diet ndiyo mambo yote. Asubuhi ninapata ki yoghurt kidogo cha 1.25 grams.
Mchana grilled fish with salad na maji
In between apples na oranges
Jioni mchemsho wa kuku wa kienyeji vipande viwili au mayai mawili ya kuchemsha na salad
Kunywa maji mengi
Sasa hivi nimefika 78 lakini aim ni kufika 70
Vipi madam ulifanikiwa kufika 70 ???
 
Back
Top Bottom