Msaada: Nitumie nini kama kuta za choo?

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,735
2,686
Salaam wanajukwaa.

Nahitaji ushauri na uzoefu juu ya jambo hili. Nahitaji kujenga choo kidogo cha kisasa pasipo kutumia tofali kwenye kuta. Chemba ipo tayari na sink zipo tayari, kinachoniwazisha ni kitu gani (material) ninayoweza kutumia kama kuta ambayo inasafishika kirahisi kama ilivyo tiles (water proof). Material hiyo iwe inapatikana hapa Tanzania.

Sakafu nitaweka tiles na sink nita set kawaida, ila kuta ndo zinaniwazisha. Nakaribisha mchango wenu wa mawazo na uzoefu wadau.
NB: Sababu kuu ni kwamba kwenye eneo husika panaruhusiwa kujengwa vitu vya muda mfupi tuu. Tofali ni marufuku. Chemba ipo karibu na eneo.
 
Tumia kioo kigumu kisichoruhusu kuona ukiwa nje wala ndani
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Kwanini ni marufuku kujenga permanent?

Na kama ni hivyo kwanini uendelee kujenga hapo?
 
Naomba nichomekee kidogo kwenye uzi wako mkuu
Hivi ni kwa nini hawa watengenezaji wa plastic kama (kiboko,Jambo,Cello.etc)hawaoni fursa kama hii au kutengeneza milango ya plastic ambayo ingefaa kukaa chooni ama sehemu zenye majimaji!?
Pvc zinafanya kazi vizuri tu. Frame unaweka za alminium.
 
Naomba nichomekee kidogo kwenye uzi wako mkuu
Hivi ni kwa nini hawa watengenezaji wa plastic kama (kiboko,Jambo,Cello.etc)hawaoni fursa kama hii au kutengeneza milango ya plastic ambayo ingefaa kukaa chooni ama sehemu zenye majimaji!?
Kuna Technology ya PVC unaweza tengeneza Milango na madirisha, ipo nchini siku nyingi!
 
Kwanini ni marufuku kujenga permanent?
Na kama ni hivyo kwanini uendelee kujenga hapo?
Mkuu jiongeze. Inaweza kuwa nyumba ya kupanga. Vyoo ni vya kushare. Ila jamaa anataka ajijengee chake. Wewe cha msingi jibu swali usitake kudadisi mengineyo.
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Asanteni sana kwa mliochangia uzi kwa kunipa ushauri.

Nimeufanyia kazi ushauri wenu na kazi ilikuwa rahisi sana. Nilichukua mbao asubuhi na kutengeneza kibanda mraba cha 4ftx4ft (kama vile vya mawakala wa pesa) na kuacha 3ft sehemu ya mlango.

Kisha nikapachika pvc kwenye kuta zote jioni hii kwakuzivalisha kwenye zile lock zake kusha nikazifunga kwa screw. Kimekuwa kizuri sana utadhani ni tiles na ukimwaga maji yanateleza tuu. Kesho napumzika, keshokutwa nakamilisha kazi.
 
Mkuu jiongeze. Inaweza kuwa nyumba ya kupanga. Vyoo ni vya kushare. Ila jamaa anataka ajijengee chake. Wewe cha msingi jibu swali usitake kudadisi mengineyo.
Umemjibu sahihi kabisa mkuu. Ni sehemu niliyopanga ya biashara
 
Asanteni sana kwa mliochangia uzi kwa kunipa ushauri.

Nimeufanyia kazi ushauri wenu na kazi ilikuwa rahisi sana. Nilichukua mbao asubuhi na kutengeneza kibanda mraba cha 4ftx4ft (kama vile vya mawakala wa pesa) na kuacha 3ft sehemu ya mlango.

Kisha nikapachika pvc kwenye kuta zote jioni hii kwakuzivalisha kwenye zile lock zake kusha nikazifunga kwa screw. Kimekuwa kizuri sana utadhani ni tiles na ukimwaga maji yanateleza tuu. Kesho napumzika, keshokutwa nakamilisha kazi.
Safi, changamoto mbao zikipata maji huoza. Nilijua inawezekana kutumia mbao ila aluminium ilikuwa ni bora zaidi. Labda kwa kuwa ni ghali.
 
Back
Top Bottom