Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?


Na hicho kilichopelekea mawazo kunipa tafsiri hiyo ni kipi?
 

Uchawi ni nini?

Ulivyoandika hapo ni kama umekubali kwamba jambo usilolijua ni uchawi.

Utajuaje kwamba ni uchawi wakati hujalijua?

Arthur C. Clarke alisema "any advanced technology is indistinguishable from magic".

Mababu zetu walioishi kabla ya usafiri wa ndege wangeona ndege inabeba watu na inaruka leo wangesema uchawi, wakati ni physics tu.

Utajuaje kwamba unachofikiri uchawi wewe leo si kitu kinachoweza kuelezewa vizuri tu bila ya kuhitaji habari ya uchawi?
 

Hehehehe. Nakubaliana na Arthur.
Kuna mwanasaikolojia mmoja wa Tanzania aliitwa Munga Tehenan na alikuwa Mhariri wa gazeti la Jitambue. Huyu jamaa alikuwa anafundisha hata kumuita mwanamke unayempenda kwa mazingara, unachukua unyoya wa tausi...blah blah, akawa anawasihi wanafunzi wake wajaribu tu kuona kama mambo hayo yanawezekana. Kujua na kujaribu na kufanya kitu kama hicho hakufuti maana ya kuwa ni uchawi. Kwahiyo nakiri kuwa kuna jambo ambalo leo naliona ni uchawi na kesho sitoliona hivyo lakini teknolojia kama hiyo ya kumvuta mwanamke ambaye hata hakujui kwa kuchukua unyoya wa tausi, ukaweke kwenye maji, saa flani, n.k. Halafu kesho huyo mwanamke anakuja from no where huo ni uchawi tu.
 

Inawezekana kabisa handsome boy yuko fresh ana kazi nzuri etc lakini anaogopa kutongoza.

Anaenda kwa mganga apewe dawa, mganga (mchawi/ mganga wa kunuiza) mara nyingi anatumia psychology. Anampa mavumba ya uongo na kweli, jamaa anapata ma confidence kwamba na nguvu ya uchawi, anawa approach wanawake, wanamkubalia kwa sababu ya kumkubalia yeye mwenyewe, lakini yeye anaona ni uchawi unafanya kazi.

Ni psychology tu hapo.
 
Hehehe ishakuwa ujinga tena!
Na kuna mtu kenya ameamka asubuhi na kujikuta hana sehemu zake za siri,sasa sijui nao ni ujinga au vp.

Ujinga ni neno tu. Sisi wote ni wajinga, kwa jambo moja au jingine. Kitu usipokijua una ujinga nacho. Ignorance.

Amejikuta hana sehemu za siri kivipi? Imethibitishwa vipi?

Siku hizi stories kibao watu wanataka kuuza magazeti.

Hii habari kabla ya kuimeza nzimanzima umeithibitisha vipi?

Unajuaje kwamba alikuwa nazo kabla mpaka leo useme leo amejikuta hana sehemu za siri, hata kama kweli leo hana sehemu zake za siri?

Hata kama alikuwa nazo jana na leo hana, is that enough to say "this is uchawi"?. How do you get to this conclusion before knowing what happenned?
 
Hey

Di you apply the blood and and Name of Jesus. Please give us some updates.
 
Mtu ana supernatural gani?

Wapi umepata habari hii?

Comprehension please!

Usipende kuamini reference saana wakati mifano ipo kwako wewe
Mifano ya nguvu asili kutoka kwako ni kuhisi kitu fulani kitatokea then kinatokea kweli...,
Umeota umeona pesa nyingi then baada ya siku kadhaa unafanikiwa katika hilo
 
Herbalist ni utaalamu wa dawa kwa kutumia mimea/ mitishamba. This is chemistry and biology. Uchawi ni kuamini supernatural forces.

Mkuu umefika pazuri kabisa

Hizo supernatural forces zipoje???
 


Kujua ni vp mtu anafanya hadi inaonekana kweli anakata kichwa cha mtu haifanyi iwe kitendo kile si cha kichawi tena.
 
Usipende kuamini reference saana wakati mifano ipo kwako wewe
Mifano ya nguvu asili kutoka kwako ni kuhisi kitu fulani kitatokea then kinatokea kweli...,
Umeota umeona pesa nyingi then baada ya siku kadhaa unafanikiwa katika hilo

Nguvu asili ndiyo supernatural?

Hivi unaelewa hata maana ya supernatural?

Unafahamu ndoto zinaanzaanzaje na kwa nini si ajabu mtu kuota unapata pesa nyingi halafu baada ya siku nyingi ukafanikiwa katika hilo?
 
Kujua ni vp mtu anafanya hadi inaonekana kweli anakata kichwa cha mtu haifanyi iwe kitendo kile si cha kichawi tena.

Hapa ulichoandika ni sawa na kuandika "Kujua kwamba movies zinakuwa na dummies wanaokatwa vichwa na kufanya ionekane mtu kakatwa kichwa haifanyi kitendo kile si cha kichawi tena".
 
Hapa ulichoandika ni sawa na kuandika "Kujua kwamba movies zinakuwa na dummies wanaokatwa vichwa na kufanya ionekane mtu kakatwa kichwa haifanyi kitendo kile si cha kichawi tena".

We unazungumzia movie?
 
Nguvu asili ndiyo supernatural?

Hivi unaelewa hata maana ya supernatural?

Unafahamu ndoto zinaanzaanzaje na kwa nini si ajabu mtu kuota unapata pesa nyingi halafu baada ya siku nyingi ukafanikiwa katika hilo?

Tusiende mbali sana mkuu kwa upeo wako super natural forces ni zipi ???
 
We unazungumzia movie?

Unajuaje kwamba utundu ule ule unaotumiwa kwenye movies hauwezi kubadilishwa kidogo tu na kufanywa kwenye live audience ukakufanya uamini kwamba ni uchawi.

Ushawahi kuona watu wanavyoliwa hela kwenye mchezo wa karata tatu?

Kama ushawahi kuna uchawi pale?

Mazingaombwe ni karata tatu tu, mengine yanaweza kuwa complex zaidi yakataka more preparation and involvement, lakini principle ni ile ile tu.
 
Tusiende mbali sana mkuu kwa upeo wako super natural forces ni zipi ???

Super natural forces hazipo. Hazijawa established kwamba zipo, na ili kusema zipo inabidi ziwe established kwanza.

Forces zote walizofikiri watu wa zamani ni supernatural ilikuwa kwa sababu ya ujinga tu, tulivyokuja kujifunza zaidi tumeelewa kwamba ni natural na si supernatural.

This shows that there is a clear convergence towards defining all phenomena from a natural perspective and not needing the supernatural, especially if it is a blatant lumping together of almost all the unknown, lazily, into a pile of "uchawi" or "mungu".

Ndiyo habari ile ile ya watu wa zamani kufikiri mtu anayeweza kutabiri kupatwa kwa mwezi au jua ni mchawi, kumbe ni astronomy tu.

Au watu walifikiri anga kupiga radi ni mungu kakasirika anafoka, kumbe ni mambo ya umeme angani tu.

Sasa, hata vile ambavyo hatuvielewi vinatokeaje, tufanye juhudi ya kuvichunguza na kuvielewa.Vinaeleweka within a natural context tu. Hakuna sababu ya kukimbilia supernatural wakati bado hatujui vitu vingi sana kuhusu the natural world.

Utasemaje "this is supernatural" wakati huja exhaust knowledge ya the natural world?

The word "supernatural" depicts that this has surpassed the natural, that is why it is "supernatural".

Sisi hata hatujui mwisho wa the natural world ni wapi. Kuna watu wanafanya mahesabu ya ku reconcile quantum theory na relativity mpaka leo. Mahesabu yamemshinda Einstein kuanzia miaka mia moja iliyopita mpaka analala kaburini, watu wanayafanya mpaka leo hawajaweza kuyamaliza. Na haya yote yanahusiana na the natural world.

Sasa kabla hatujamaliza haya ya natural world unapata wapi confidence ya kusema "this is supernatural"?
 
Duh hapo ni kuomba MUNGU tu kama ukiingia kwny mtandao huo lazima uwe mchawi kumshinda huyo mama
 

Siwezi kuitazama kwa sasa, nitaitazama baadaye.

Kwa hiyo ukionyeshwa video Amitab Bachchan karuka ghorofa mia utaamini kwamba karuka kweli?

Na nimekuuliza, hata kama ni kweli jamaa kapoteza hizo sehemu zake za siri, kitu gani kitafanya jibu automatically liwe uchawi na si kitu kingine chochote, hata kama kiwe improbable namna gani ?

After all watu siku hizi wanafanya mpaka sex change surgery, wanaume wanaondoa dhakari na kuota maziwa!

Hiyo nayo ni uchawi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…