Pole sana ndugu yangu, mimi naanza kwanza kukuchambulia hayo majibu uliyopatiwa, nakuchambulia ili uwelewe unasumbuliwa na nini. Maandishi ya rangi ya blue nitayo yaweka ndio maanidshi yaliyo andikwa kwenye karatasi yako, kwa hiyo nitakuwa nayafasiri na kukuelezea kwa kina. Halafu baada ya hapo utanitafuta kwa ajili ya tiba kama utapendezwa.
...............
Uchambuzi wa jumla wa sifa za shahawa ndio huitwa (Macroscopic Examination) , hujumuisha ujazo wa shahawa, pH, na rangi ya shahawa
Macroscopic Examination = Uchambuzi wa jumla
(a) Apperance -> homogeneous gray, opalescent colour
= Muonekano wa mbegu zako kwa sehemu kubwa zina rangi ya kijivu na zingine hazina rangi (Opalescent) ina maana isiyo na rangi au nyeupe kama opal. Ambapo ndio hali ya kawaida mbegu zinatakiwa kuwa namna hiyo.
ISIYOKAWAIDA Mfano Rangi nyekundu au kahawia inaweza kuonyesha uwepo wa damu katika maji ya uzazi. Mwonekano mweupe, pia wenye mawimbi unaweza kuonyesha maambukizi.
(b) Volume -> 8 mls
= Ujazo wa mbegu zako ni Mils 8 kwa bao moja, ambapo ni hali ya kawaida bado lakini yenye utata kwasababu unazalisha mbegu nyingi sana kwa mils 8 kwa bao moja.
Kiwango cha ujazo wa kawaida huanza Mils 1.5 hadi 7.6 mL. Kwa hiyo hapa kuna tatizo la kutoa maji mengi kuliko kawaida wakati wa kumwaga bao, hali hii hufahamika kitaalamu kama (hyperspermia). Tatizo hili linaweza kuathiri uzazi wa mtu, lakini si mara zote. Baadhi ya wanaume ambao wana ujazo mkubwa sana wa shahawa huwa wana mbegu chache kuliko kawaida katika maji wanayomwaga. Ambapo kunapunguza uwezekano wa mbegu hizo chache kurutubisha yai moja la mkeo.
(c) PH -> 8.5
= PH ni kiwango cha asidi kwenye mbegu zako za uzazi ambapo ni 8.5. Kiwango cha pH cha kawaida ni 7.2 hadi 8.0. Kiwango cha chini cha pH kinamaanisha kuwa una shahawa zenye tindikali. Kiwango cha juu cha pH inamaanisha kuwa ni alkali yaani besi. PH isiyo ya kawaida inaweza kuathiri afya ya mbegu za uzazi kutokana na jinsi inavyosonga mbele.
Hiyo ni hatua ya kwanza ya kipimo, tunakuja hatua ya pili...................
...........
Uchunguzi wa shahawa kwa kutumia darubini (Microscopic examination), katika kipimo hichi kinapambanua mjongeo wa mbegu (motility), idadi ya mbegu (sperm number), mnato wa mbegu (Viscosity) na muundo wa mbegu (Morphology) kama ilivyoainishwa kwenye karatasi lako.
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo
Microscopic examination = Uchunguzi wa shahawa kwa kutumia darubini, majibu ni kama ifuatavyo
(a) Motility
-> spermatozoa moving sluggish:
Mjongeo wa mbegu ziko polepole sana tena kwa uvivu, mjongeo wa mbegu zako upo chini hivyo kutokuwa na uwezo wa kusonga haraka na kwa ufanisi kuelekea yai la mwanamke.
->Progressive motility -> Spermatozoa has no active motility (Mbegu hazina uwezo wa kusonga mbele, zisizo na mpangilio katika mwendo wa kusonga mbele)
->Non progressive motility (Mbegu hazisongi mbele zinazunguka hapo hapo tu lakini hazisongi mbele kwa mstari ulio nyooka, hizi ni mbegu ambazo huogelea kwenye miduara iliyobana sana)
Fahamu kidogo kwanza kuhusu mjongeo wa mbegu iko hivi,
Mwendo kasi wa mbegu za kiume (sperm motility) ni moja ya tabia muhimu zaidi ili kutimiza lengo lake kuu, ambalo ni kufikia na kurutubisha yai la mwanamke, baada ya mbegu kukomazwa na kuhifadhiwa kwenye kifuko cha korodani (epididymis) hupatiwa uwezo wa kusonga mbele baada ya kutolewa. Aina ya kwanza ya mjongeo ''activated progressive motility'' ni mfano wa mwendo wa bendera ya ulinganifu ambayo husababisha mbegu kwenda mbele kwa harakati zaidi. Aina ya pili ya mjongeo ''hyperactivated motility'' huanza baada ya kipindi cha muda katika njia ya uzazi ya kike, mjongeo huwa ni wakupinda zaidi ya mwendo wa bendera kwa urefu wa kupanda na kushuka na kujipinda kama mjeledi, hali hii hufanyika wakati wa urutubishaji ambapo mbegu hujikata mkia wake, na kichwa huingia kwenye yai la mwanamke.
(b) Sperm number -> 20% spermatozoa per unit volume
Idadi ya mbegu katika maji uliyotoa kuna asilimia 20% ya mbegu kwa ujazo. Idadi ya mbegu kwa kawaida huanzia milioni 15 hadi zaidi ya mbegu milioni 200 kwa mililita ya shahawa. Unachukuliwa kuwa na idadi ndogo ya mbegu ikiwa una manii chini ya milioni 15 kwa mililita.
(b) Viscosity -> Has abnormal thread length 2cm and above
Maji yako ya mbegu za uzazi ni mazito na yana nata sana kiasi kwamba yanaweza kuvutika hadi urefu wa sentimita mbili. Iko hivi ndugu yangu uzito wa mbegu au shahawa hufahamika kama (Viscosity) ni ile hali ya mnato wa mbegu za uzazi kutokana na ute ute, mnato au uzito unaweza kuwa chini (dhaifu) au unaweza kuwa juu, kikawaida mbegu zinatakiwa kuwa na majimaji ili ziweze kutembea ipasavyo. Kwa hiyo 'Sperm Viscosity' ni mnato wa mbegu. 'Hyperviscosity' ni mbegu zinazo nata sana au nzito kupita kiasi. 'Hypoviscosity' mbegu zisizo na mnato, nyepesi kupita kiasi. Mbegu zikinata sana au kuwa nzito sana ni shida kwa maana hazitoweza kupita ili kwenda kutungisha yai kutokana na mnato huo.
(c) Morphology
->Has normal morphology -> Has oval heads and single tail piece
(Morphology ni maumbile ya mbegu zako za uzazi, mbegu zako zipo normal kimaumbile yaani zipo kawaida kwasababu zina vichwa vya mviringo na kipande cha mkia mmoja.
Fahamu jambo moja kwanza.
Uwezo wa mbegu ya kiume kurutubisha yai la mwanamke hufahamika kama (capacitation), inategemea na umbile la mbegu hiyo (morphology), utendaji kazi wake (physiology) na uwezo wake wa ndani kwenye vinasaba (biochemical changes). Mbegu hupata misukosuko sana wakati wa kulitoboa yai la mwanamke kwenye eneo la yai au mlango wa yai panapoitwa (cumulus oophorus) na sehemu au mlango mwingine wa yai unaoitwa (corona radiata) na sehemu nyingine inaitwa (zona pellucida) hayo yote ni maeneo maalum ya yai la mwanamke ambapo mbegu ya mwanaume hutegemea kuingia kupitia eneo hizo. Maeneo hayo yakiwa na hitilafu pia ni dhahiri mbegu haitaweza kuingia kwenye yai la mwanamke, au mbegu ikiwa na hitilafu yoyote haitaruhusiwa au kuwa na uwezo wa kupita kwenye milango hiyo.
Hayo ndio majibu yako, nadhani umeelewa sasa nini kinakusumbua. Usisite kuwasiliana nasi tafadhali