Msaada: Nimetekwa China

CCM yenyewe wapo hoi.

wakufuate hadi china wewe nani?

Wakati mwingine msitake kusingizia watu kwa kuwataja CCM.

Ni kweli CCM haina Mvuto kwa sasa.

Lakini si kwa kukufuatilia namna hii kama kukumaliza wangekumaliza huko huko Iringa.


Sio mbaya inaweza kuwa ni mwanzo wa kuchanganyikiwa.

Pole. Kama ni hivyo wakina Lisu waseme nini?
 
Wewe ni Deo Kisandu....
Nimetambua uandishi wako mkuu....
Jitahidi utafute tiba ya magonjwa ya akili haraka sana kabla hali haijawa mbaya zaidi....
 
Umenikumbusha stori ya Mzee Jackson Makweta alichofanywa na hao jamaa kwa kuwa alikuwa na nyota ya kuwa Mukulu...
Mzee mpaka dakika ya mwisho alikufa analia Tanzania yangu, Tanzania yangu.
Yeye aliipenda Tanzania ila "wazee wa kamati ya ufundi" wa nchi walimpenda zaidi.

Nimewahi kukutana na jamaa wa kaliba yako Musoma huko, yeye naye "wazee wa kamati ya ufundi" walimfanyia kitu mbaya.
Wakamchomoa ndani wakampeleka ofisi kubwa akawa mtumishi wa bila malipo, mule ndani wakamuweka mzungu akaendelea kula msuli UDSM.
Dogo ana masters kali kwa sasa, ukimuona utadhani aliishia darasa la nne.

Alinisimulia vitu vingi sana.
Ila kizito ni kuwa "wazee" walikuwa wanaitumia nyota yake kwenye mambo ya "Public Administration" pale jumba jeupe.
Walipoona nyota imewanogea wakaamua kumnyofoamo mazima.

Hapa JF ni vigumu kupata msaada kwa kuwa wengi mambo ya kiroho yamewapita kando sana.
Ila vita uliyo nayo ni kubwa aisee.
Jitadi kusali sana, mana inaonekana wameshindwa kukuondoa ili wajimilikishe nyota yako sasa wanataka uwauzie ulicho nacho lakini umekuwa mgumu kufikia bei.

Siku utakapo kula tu kiapo cha kuingia chama jekundu, ndio utakuwa umejirestisha in pisi mazima.
Ni hayo tu mkuu.
 
CCM ina mabaya yake lakini kwa hili tunaisingizia kama ilivyo kwa mkubwa jalala
 
dogo acha undezi hizi akili ni zawana. ccm sasa sijui wewe mpinzani umezitoa wapi
 
Umemshauri vema.
Huyu ana msongo mkubwa wa mawazo kwa kufanya vibaya kielimu. Huko chuo kote anakopita anakatwa vibaya ndio inampa shida anatafuta mtu wa kumlaumu kwa matatizo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…