Habari wakuu
Ninajishughulisha na biashara ya m- pesa na tigo pesa ( haina mda mrefu) ambapo kwa siku za nyuma niliajiri kijana aliyehudumia hapo hadi mwisho wa mwezi wa pili 28/02/2019. Baada ya huyo kijana kudai anataka kwenda kwao kusalimia nililazimika kutafuta mtu wa kusimamia ofisi! Nilipata kijana mwingine ambaye alianza rasmi kazi 01/03/2019 nikiwa naye nikimpa maelekezo namna ya kuendesha biashara.
Juzi tarehe 03 nilisafiri kidogo kwenda kuona familia na kumwacha peke yake Jana alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama tigo makao makuu na kumpa taarifa juu ya laini ya tigo (till)kuwa usajili haujakamilika na kumweleza kuwa lain inaweza kufungwa na kumtaka akamilishe usajili huyo jamaa alimpanga dogo kwa kumpa maelekeo mara kadhaa na kufanikiwa kutumiwa pesa kutoka tigo pesa, na hatimaye kumchoa kwenye M-Pesa pia.
Dogo alifanya miamala mara kadhaa bila kujua kwa kufuata maelekezo ya huyo jamaa anayejiita huduma kwa wateja makao makuu baada ya kugundua kuingizwa kingi alinipa taarifa SAA tatu usiku nkalazimika kuja Leo kufatilia na kubaini utapeli uongo.
Nilipiga simu vodacom wakaniambia pesa ilitolewa ndani ya dakika tano na wakanijbu hawana msaada mwingine kwani pesa ikishatolewa hawana uwezo kwa kuirudisha
Nilienda polisi kuripoti na kuandikiwa RB na kuambiwa nirudi kesho yake ili nipewe mpelelezi wa suala langu!
SWALI: Je, kuna uwezekano wa kufuatilia hadi kwa wakala aliyetoa pesa na kumkamata mhalifu?
Je, ni changamoto zipi ninaweza kupata katka kutoa ushahidi kwani hizo tills zote hazijasajiliwa kwa majina yangu kwani nilinunua kwa watu( mawakala wanazoziuza)?
.
.
Nakaribisha mawazo yenu wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app