callmeGhost
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 278
- 832
Pole Sana. Mimi nina two incidents.Habari wakuu
Ninajishughulisha na biashara ya m- pesa na tigo pesa ( haina mda mrefu) ambapo kwa siku za nyuma niliajiri kijana aliyehudumia hapo hadi mwisho wa mwezi wa pili 28/02/2019. Baada ya huyo kijana kudai anataka kwenda kwao kusalimia nililazimika kutafuta mtu wa kusimamia ofisi! Nilipata kijana mwingine ambaye alianza rasmi kazi 01/03/2019 nikiwa naye nikimpa maelekezo namna ya kuendesha biashara.
Juzi tarehe 03 nilisafiri kidogo kwenda kuona familia na kumwacha peke yake Jana alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama tigo makao makuu na kumpa taarifa juu ya laini ya tigo (till)kuwa usajili haujakamilika na kumweleza kuwa lain inaweza kufungwa na kumtaka akamilishe usajili huyo jamaa alimpanga dogo kwa kumpa maelekeo mara kadhaa na kufanikiwa kutumiwa pesa kutoka tigo pesa, na hatimaye kumchoa kwenye m- pesa pia.
Dogo alifanya miamala mara kadhaa bila kujua kwa kufuata maelekezo ya huyo jamaa anayejiita huduma kwa wateja makao makuu baada ya kugundua kuingizwa kingi alinipa taarifa SAA tatu usiku nkalazimika kuja Leo kufatilia na kubaini utapeli uongo.
Nilipiga simu vodacom wakaniambia pesa ilitolewa ndani ya dakika tano na wakanijbu hawana msaada mwingine kwani pesa ikishatolewa hawana uwezo kwa kuirudisha
Nilienda polisi kuripoti na kuandikiwa RB na kuambiwa nirudi kesho yake ili nipewe mpelelezi wa suala langu!
SWALI: Je, kuna uwezekano wa kufuatilia hadi kwa wakala aliyetoa pesa na kumkamata mhalifu?
Je, ni changamoto zipi ninaweza kupata katka kutoa ushahidi kwani hizo tills zote hazijasajiliwa kwa majina yangu kwani nilinunua kwa watu( mawakala wanazoziuza)?
.
.
Nakaribisha mawazo yenu wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app
1)
Miezi michache iliyopita nilikuwa Dar, mtaani kwetu actually. Kuna mdada fulani alikuja na begi akamwambia wakala 'nataka uniingizie laki 2 kwenye hii number...' yule wakala ni wakitaa na wateja wengi asilimia kubwa wanaishi humo mtaani kwahiyo ana amini Sana watu, mpaka Kuna cases nyingine nampigiaga simu anikopeshe laki MPESA, so ana trust Sana. Kwasababu hiyo, akaingiza zile laki 2, akitegemea yule dada atatoa hela papo hapo.
Yule dada ni mgeni mtaani. Yule dada akasema subiri naingiziwa laki 5 nakupa
. Kwasababu ni mgeni, yule wakala akawa very alert akajaribu kumuuliza sasa nimeingiza hii laki 2 nikijua una hela hapo hapo, kwanini usingesubiri uingiziwe. Bhasi akawa mpole. Mimi niliwaacha dukani baada ya Kama masaa mawili narudi Tena, nilikuta yule dada anakula makofi, alafu watu kibao. Mimi sio mtu wa mob kabisa. Nikaghaili, badala yake nikaenda pembeni kwenye kibar flani. Hapo ndio nitapata habari.Yule dada alipigiwa simu na watu wanajiita Vodacom makao makuu(note mwenyewe walishanipigia nikawaambia tumieni number za office nitawajibu). Hawa 'voda' wakamwambia kashinda laki 5. Hivyo anatakiwa ajibu maswali Kama kwenye account yake Kuna TSH ngapi, number za mwisho kuwasiliana nazo nk. Mwishoni akaambiwa ili kupata bonus yako tuma laki 2, ili tuverify Kama mpesa yako iko active alafu tunakurushia laki 5 + 2 = laki 7. Kwahiyo dada wa watu akaingia kwenye line, wale watu hawakupatikana tena.
Kilichonisikitisha ni tukio. Sawa maybe alietapeliwa nae kaonekana mwizi. I get it. Yule dada Kwanza ni mfanyakazi wa ndani. Bosi wake kusikia hilo akamkana akasema na aondoke kabisa. Je kwanini asingelipa akamkata kwenye mshahara? Yule dada alikuwa kavaa sketi fupi, ana shape fulani hivi, usoni havutii Sana(beauty is in the eye of the beholder); wakaka walikuwa wanamshika shika... Yani Ile ilikuwa sexual harassment. Mtu wamemlaza kwenye mchanga alafu kila mtu anampiga kibao, mwingine anaoitisha mkono chini ya sketi
. Kwasababu mjumbe alikuwa karibu tukamjulisha. Akaja. Watu wakajitolea eti walale nae alafu watalipa
wengine eti ungekuwa mzuri ningekusaidia. Jamani. Fast forward police walishindwa kufanya chochote. Dada alishinda siku 3 polisi. Mpaka polisi wakamwambia wakala amsaidie TENA hela ya nauli arudi kijijini maana yule dada Hana pakukimbilia. Disappointment.2)
Kwenye harakati zakutafuta laptop, niliona hii laptop kupatana yenye dhamani ya mil 3 Ila muuzaji anauza laki 7. Mnajua tunavyopenda kusave, Tena kwa sisi vijana ambao ndio Kwanza tunausoma mchezo hata hatuna pressure yakuwaza fees. Bhasi nikampigia. Akanipanga kweli, oh Zanzibar hatuna ushuru ndio maana anauza cheap. Nikawa sold. Huyu Kaka aliniaminisha akaniambia naweza fika Zanzibar au ananitumia mzigi kwa elfu 30 tu. To be honest moyo ukawa mzito. Nikaseme nikirudi likizo ya mwakani nitanunua Kama sitonunua huko chuo.
Kipindi hicho moja ya rafiki zangu nae alikuwa ana haunt laptop. Nikampa habari. Ila nikampa pia my doubts. Nikamwambia Bora twende physically, kwani tunaweza pendezewa na kingine humo dukani. Tukaelewana. Siku 3 baadae akanipigia simu. Akaniambia eh bhana Ghost Mimi naenda Zanzibar kesho. Nahitaji ile laptop. Nikamwambia sawa safari njema. Siku hiyo hiyo mida ya saa kumi na moja, nikakuta missed calls kibao. Kwani nilikuwa nimelala. Nikampigia. 'Ghost jamaa hapatikani.' Nikamwambia si safari kesho, subiri kesho. Akasema 'Nimetuma laki 7 nipo Kivukoni masaa manne Sasa simpati' kuh!!!
Kiukweli sikuwa alerted Sana. Cause huyu jamaa alikuwa akimalizia sentensi zake na 'mimi muislamu siwezi kukutapeli'. Na kwa my experience marafiki zangu waislamu wakiniambia kitu mostly it's true. Hawanaga chenga Kama ndugu zangu wengine
. Yule rafiki yangu akaondoka Kivukoni saa tatu usiku. Nikamwambia tusubiri kesho...Fast forward. Ikajulikana kweli duka lipo Zanzibar. Hapa nimemtumia rafiki yangu alieenda kula Bata huko. Police waligoma eti bado upelelezi. Lakini hela ilitolewa CRDB Dodoma. Jina lilosajiliwa kwenye simu tofauti na anavyojiita. Bank ilisoma jina lingine pia. Nilimwambia rafiki yangu aulizie dukani Kama wanamjua. Wakasema hawamjui. Point is police walipotezea hii issue. Kila siku bado upelelezi. Mpaka leo hii nikimtext yule Kaka anajibu na anataka kuniuzia computer za 2m+ kwa laki 5. That means anaiba na serikali haimfanyi chochote. Raisi Magufuli, tunaomba unwambie IGP hii shida, ule mtambo wa TCRA faida yake Nini? Maana ulikuwa unafanya kazi toka enzi za Kikwete.
P.s msitume hela remotely... Pia hata Kama ni physical muandike kwa maandishi. Na hii sio guarantee hela yako ipo safe but it's better than nothing.
-callmeGhost
Sent using Jamii Forums mobile app