Msaada: Nimepoteza laini ya uwakala(m-pesa)

Jiran mwema

Senior Member
Nov 7, 2015
164
103
Habar zenu wana Jamvi
Kama kichwa cha uzi hapo juu,Nimepotelewa na lain yangu ya uwakala na kuna pesa ndan yake nashindwa nifanyeje ili niirudishe.
Kwa wenye uelewa tafadhar nipeni mwanga.
Note:Hiyo lain nilinunua kwa mtu hivo nyaraka zake sina maana(Haikua na Jina langu).
 
Pengine haikuwa ridhki yako, ushauri wangu tengeneza urafiki na mtu wa vodashop haraka iwezekanavyo au tafuta mtu mwenye urafiki na mtu wa vodashop atakusaidia
 
Kweli mtihani ila wasiliana na aliekuuzia muelezee kuhusu kupotea kwa iyo laini muombe akupe hizo nyaraka ili uweze kwenda kuirenew..

Au unaweza kwenda Vodacom shop ukawaekeza tatizo usikilize watakupa procedure gani zakufwata
NB: Voda uciwape data zozote za Laini iliyopotea wew waelezee scenario wakupe maelekezo nini chakufanya,
 
Pengine haikuwa ridhki yako, ushauri wangu tengeneza urafiki na mtu wa vodashop haraka iwezekanavyo au tafuta mtu mwenye urafiki na mtu wa vodashop atakusaidia
Mtu wa voda shop hawezi msaidia chochote ,hiyo ngoma mpaka Wakala wake mkuu awasiliane na voda makao makuu ,kwa hiyo apo lazima mwenye laini ahusike amtafute aliyemuuzia
 
Nenda voda makao makuu,anagalia kwenye list ya mawakala wakuu ,umjue Wakala wako mkuu ni yupo ,alafu uende uko kwanza ila duh ukipata ni ishu sana
 
Mtu wa voda shop hawezi msaidia chochote ,hiyo ngoma mpaka Wakala wake mkuu awasiliane na voda makao makuu ,kwa hiyo apo lazima mwenye laini ahusike amtafute aliyemuuzia
Anaweza ndugu mtanzania, atakuwa ni kiungo data zote wako nazo hivyo yeye ndio atacheza na system.
Viazi ndio lazima wapewe complications
 
Habar zenu wana Jamvi
Kama kichwa cha uzi hapo juu,Nimepotelewa na lain yangu ya uwakala na kuna pesa ndan yake nashindwa nifanyeje ili niirudishe.
Kwa wenye uelewa tafadhar nipeni mwanga.
Note:Hiyo lain nilinunua kwa mtu hivo nyaraka zake sina maana(Haikua na Jina langu).
Kama uko Dar nenda Makao makuu ya Voda (Mlimani City). Wambie ukweli kuhusu umiliki wako wa laini, wambie huna leseni wala TIN wao watakupa mawasiliano ya wakala mkuu(ambaye wewe uko chini yake), ukishafika kwa wakala mkuu atakupa barua ya utambulisho na voda pia watakupa barua ya utambulisho, utaenda polisi watakupa loss report hivyo vyote utavibeba na kuvipeleka voda watafanya michakato yao kisha laini yako utapewa, ukumbuke kua na taarifa za kiasi cha pesa kilichokuwemo kwenye laini maana utaulizwa.

Itachukua kama 1-2 weeks mpaka kuipata.

Unaweza kunitafuta PM nikupe mawasiliano ya mtu anayeweza kukusaidia muongozo yuko pale ofisini (kitengo cha Mpesa).
 
Kama uko Dar nenda Makao makuu ya Voda (Mlimani City). Ukweli kuhusu umiliki wako wa laini, wambie huna leseni wala TIN wao watakupa mawasiliano ya wakala mkuu(ambaye wewe uko chini yake), ukishafika kwa wakala mkuu atakupa barua ya utambulisho, utaenda polisi watakupa loss report hivyo vyote utavibeba na kuvipeleka voda watafanya michakato yao kisha laini yako utapewa, ukumbuke kua na taarifa za kiasi cha pesa kilichokuwemo kwenye laini maana utaulizwa.

Itachukua kama 1-2 weeks mpaka kuipata.
Habar zenu wana Jamvi
Kama kichwa cha uzi hapo juu,Nimepotelewa na lain yangu ya uwakala na kuna pesa ndan yake nashindwa nifanyeje ili niirudishe.
Kwa wenye uelewa tafadhar nipeni mwanga.
Note:Hiyo lain nilinunua kwa mtu hivo nyaraka zake sina maana(Haikua na Jina langu).
du kwa kweli ni kazi yaani kwa ushauri wangu anza upya kwani mimi ilishawahi kunitokeaa ni ngumu sana kuipata
 
Wafanyakazi wa voda wanavyopenda RUSHWA, jiandae mkuu. Ila mtafute jamaa aliyekuuzia laini akusaidie ID yake. Ingekuwa tigo ungepata hata bila ID ya huyo aliyekuuzia. Unawapelekea ID yako na maelezo full ya laini ila lazima upitie kwa wakala mkuu akupe barua ya utambulisho ndiyo unaenda nayo huko wana renew laini.

Voda kumejaa mihuni, siwezi shauri. Labda umtafute aliyekuuzia laini iwe ndio starter point
 
du kwa kweli ni kazi yaani kwa ushauri wangu anza upya kwani mimi ilishawahi kunitokeaa ni ngumu sana kuipata
Sio ngumu usimtishe.
Mimi nilipoteza laini ya uwakala ambayo haikua na jina langu, ilikua na pesa laki 8, tena laini mbili zote zilipotea (Sim 1 na Management Sim). Nilifatilia baada ya wiki moja ikawa tayari nikapigiwa simu nikaenda kuchukua na hela zangu zikiwemo kama kawaida
 
Kama uko Dar nenda Makao makuu ya Voda (Mlimani City). Wambie ukweli kuhusu umiliki wako wa laini, wambie huna leseni wala TIN wao watakupa mawasiliano ya wakala mkuu(ambaye wewe uko chini yake), ukishafika kwa wakala mkuu atakupa barua ya utambulisho na voda pia watakupa barua ya utambulisho, utaenda polisi watakupa loss report hivyo vyote utavibeba na kuvipeleka voda watafanya michakato yao kisha laini yako utapewa, ukumbuke kua na taarifa za kiasi cha pesa kilichokuwemo kwenye laini maana utaulizwa.

Itachukua kama 1-2 weeks mpaka kuipata.

Unaweza kunitafuta PM nikupe mawasiliano ya mtu anayeweza kukusaidia muongozo yuko pale ofisini (kitengo cha Mpesa).
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom