Msaada nimepoteza ladha ya chakula na harufu

Endelea kutumia dawa na mazoezi mungu atakusaidia Wala usiwe na mawazo
Unajua mawazo muda mwingine hayakwepi imagine kuna mtu kukosa kunusa siku mbili tu hofu inamjaa sasa mie ambae ni week ya tatu sinusi wala sipati ladha ya chakula napokutana na ujumbe kama huo kuna namna kichwa inawaza mkuu [emoji23][emoji23]
 
Asante nieleweshe mafusho ni nini? Toka mwanzo wa uzi nakutana na neno mafusho ni nini hiki mkuu. Hapo kwenye malimao tangawizi kitunguu saumu nachanganya na blendi nakunywa kama juice ama
Unachukua mchaichai, majani ya muembe, majani ya mvumbasi, majani ya mpera, majani ya mdimu, muarobaini, maganda ya limao, unachanganya unaweka kwenye moto mpk yachemke unachukua shuka unavua shati unajifunika na hiyo sufuria yenye huo mchanganyiko kwa dk 10 huku mdomo umeacha wazi na macho umefumba, pia unakuwa na mwiko kwa ajili ya kugeuza geuza pindi mvuke unapopungua, unafanya kwa siku mara mbili kwa siku kadhaa utaona mabadiliko.
 
Sawa kabisa nimekupata mkuu, nimefikiria na kufanya mazoezi walau nikimbie km hata mbili naporudi nafanya mafusho. Asante sana kwa muongozo
 
Unajua mawazo muda mwingine hayakwepi imagine kuna mtu kukosa kunusa siku mbili tu hofu inamjaa sasa mie ambae ni week ya tatu sinusi wala sipati ladha ya chakula napokutana na ujumbe kama huo kuna namna kichwa inawaza mkuu [emoji23][emoji23]
Ni kweli ila nilichojifunza mawazo ndio changamoto kubwa inatutesa hususan ukijiona unadalili hizi ila naamini utaakaa sawa tu sijajua unatumia dawa gan ila mazoezi pia jitahidi ili kuzifanya Neva ziamke
 
Sawa kabisa nimekupata mkuu, nimefikiria na kufanya mazoezi walau nikimbie km hata mbili naporudi nafanya mafusho. Asante sana kwa muongozo
Pia chukua tangawizi na kitunguusaumu vilivyosagwa changanya na pilipili mtama chemsha pamoja kisa chuja changanya na limao na asali kunywa siku Mara mbili utakuja kunishukuru
 
pole sana mkuu wangu..naomba nikuulize maswali machache
●je hupati homa?(mwili kuchemka)
●Je hujaugua mafua au kikohozi hivi karibuni?...
Hii situation nilipitia kama weak mbili nyuma iv ila saiv niko vizur
 
Ni kweli ila nilichojifunza mawazo ndio changamoto kubwa inatutesa hususan ukijiona unadalili hizi ila naamini utaakaa sawa tu sijajua unatumia dawa gan ila mazoezi pia jitahidi ili kuzifanya Neva ziamke
Kuna post nimeandika dawa ambazo nilitumia kwa muda wa kama week mbili hivi, nikaweka na maelezo mengine. Nilitumia Azithromycin, cetrizine long, vidonge fulani sivikumbuki jina ni vya chenga chenga hivi. Nikapewa dawa ingine emisol nasal spray sijui kama nimepatia jina lake.
 
Unachukua mchaichai, majani ya muembe, majani ya mvumbasi, majani ya mpera, majani ya mdimu, muarobaini, maganda ya limao, unachanganya unaweka kwenye moto mpk yachemke unachukua shuka unavua shati unajifunika na hiyo sufuria yenye huo mchanganyiko kwa dk 10 huku mdomo umeacha wazi na macho umefumba, pia unakuwa na mwiko kwa ajili ya kugeuza geuza pindi mvuke unapopungua, unafanya kwa siku mara mbili kwa siku kadhaa utaona mabadiliko.
BUYEGI ambayo ni mafuta tete
 
dawa gani mkuu nisaidie nijue.
Hili tatizo kwasasa lipo serious snaa inabidi tu tuasaidiane dawa za asili nilizotumia mim ni Kama ifuatavyo.

Tangawizi ilochanganywa na kitunguu + pilipili mtama unachemsha pamoja badae unachuja na kuchanganya na asali unakunywa,pia nilisaga karafuu nikailoweka ktk chupa ya Lita moja ya maji huwa nakunywa nusu grass kila asubuhi na usiku + kujifukiza usisahau hivyo mchanganyiko vitakusaidia ktk kurejesha sensi ya pua na mdoomo laza (karafuu)hata kifua pia itakusaidia
 
Halafu kuna harufu fulani kali sana unaisikia inatoka kinywani ikiambatana na makohozi ...???
harufu kali ikitoka na makohozi au mafua ni covid. maana kuna kipindi nyuma hapo nilikwenda KCMC kumuona mgonjwa wa korona na barakoa nilikua nimevaa kitozi nilikumbwa na hiyo hali na homa kali nikawa natumia Action kila siku mpaka nikaja kukaa sawa.
Halafu kuna harufu fulani kali sana unaisikia inatoka kinywani ikiambatana na makohozi ...???
 
Hii hali ilinikumba wiki mbili zilizopita imepotea yenyewe sijaenda hospitali wala kunywa dawa. Nafikiri kinga zangu ziko vizuri.
 
Sijui na mm nnayo maana ninapata mafua makali saana nakosa taste na smell pia kupumua Ni shida maana pua zote zinaziba hasa wakati wa kulala Ila Sina homa
 
Naombeni ushauri Tena nataka nikachome chanjo baada ya kupata misuko suko ya uvico 19 vipi kutakua na changamoto yeyote au teyari mwili utakua umejitengenezea kinga?
 
Back
Top Bottom