Mkuu nimesoma thread nzima sijaacha comment hata moja, mimi ni muhanga wa kukosa harufu na ladha week ya tatu sasa.
Mwanzoni nilipata mafua makali sana na kifua naposema mafua makali ieleweke hivyo ni makali naweza sema mafua kama hayo nilipata mwaka juzi mwezi Nov. Mafua haya (niliyopata week tatu zilizopita) na kifua viliambatana na homa, viungo kuuma na kichwa pia.
Nilipima maralia, UTI, typhoid na majibu yalikuwa negative nikapewa dawa ya kifua na mafua. Pumzi haikua inabana ila mafua yalifanya nyakati za usiku napolala nipate shida kupumua kimsingi nilikuwa napumua kwa shida kiasi ila imani kwamba inaweza kua Covid haikumea akilini mwangu.
Nilirudi tena hospitali kwa habari ya kukosa harufu na kutopata ladha, Dr akaniambia itaisha taratibu akawa ameniandikia dawa zinaitwa Azithromycn, cetrizin long, emina sol nasal spray na dawa nyingine nimesahau jina. Hizi dawa zote nilitumia week mbili mfululizo ila shida ya kukosa ladha na harufu iko pale pale. Kwa sasa imebaki hiyo nasal spray nayo inaendea mwisho.
Kwa namna ambayo pua hazinusi wala sipati ladha hata kama napita mahali kuna mzoga sinusi wakuu... Ila nimemshangaa mleta thread anasema hakupata kunusa kwa siku mbili mimi sinusi week kadhaa. Ushauri wenu unahitajika wakuu.