Msaada: Nimeitwa kwenye Interview ya Shirika la umeme, ila naogopa wakiniuliza maswali kuhusu utendaji wa kazi zao

Kijana Jr

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
838
Mimi nimepata bahati ya kuitwa kwenye Interview ya shirika la Umeme Tanzania ila kinachonitatiza ni endapo nitaulizwa maswali yanayohusiana na utendaji kazi wao wa kila siku. Sababu sijawahi fanya nao kazi ila elimu yangu ya maswala ya Umeme ilinifanya niapply huko, kwa hiyo kwa mwenye kuweza kunipa mwongozo na nimeapply katika position ya lineman
 
sasa si wameshakuita ondoa wasiwasi ...ukiulizwa unachojua jibu usichojua sema sijui...mana kwenye hiyo taaluma sidhani kama wanavutiwa na porojo
 
Kuna watu juzi wameitwa wakapewa mtihan
Maswali ni wakaulizwa kuhusu wataje makosa ya manji
Mawaziri waliojiuzuru siku aliyokabidhiwa report maguful mara tarehe ya kusimamishwa matokeo
 
Nenda kama ipo ipo tuu.. Wewe mpaka umemeliza kusoma ulifanya nitihani mingapi? Uoga mwingine bana
 
Wachane, hata wakikunyima kazi lakini utakua umesaidia taifa. Na sometimes wanaeza kukupa kaz ili uwe sehem ya solution, lkn omba Mungu kwanza au ogea dawa kama unayo
 
Mimi nimepata bahati ya kuitwa kwenye Interview ya shirika la Umeme Tanzania ila kinachonitatiza ni endapo nitaulizwa maswali yanayohusiana na utendaji kazi wao wa kila siku. Sababu sijawahi fanya nao kazi ila elimu yangu ya maswala ya Umeme ilinifanya niapply huko, kwa hiyo kwa mwenye kuweza kunipa mwongozo na nimeapply katika position ya lineman
Utajua huko huko
 
Back
Top Bottom