Msaada: Nimeibiwa Laptop, nina namba ya simu ya mwizi

Msaada: Nimeibiwa Laptop, nina namba ya simu ya mwizi

Pole sana. Huo mwezi mmoja watakuwa wanafanya nini. Au POlisi wanatumia waganga wa kienyeji kuwanasa wahaifu



Polisi ndio wanatakiwa kuwasiliana na Tigo. Au ukisema polisi una maanisha umeripoti kwa polii binafsi na sio polisi wakiwa ofisini kiofisi. Kama umeripoti kifosii Polisi wana uwezo nadhani hata sheria inawawezesha kupata detail za mtu mwenye number fulani.

Hzo detail Hata mfanyakazi wa tigo si rahisi kukuwezesha unless anataka kukomboa laptop yako kwa kupoteza ajira yake. Polisi watajua hata IMEI No. IMEI number inawawezesha polisi kujua muhusika hata akiweka kadi ya simu nyingie mradi tu watume aombi ya kupewa detail hizo. Kwa kutumia na kupewa detai za kampuni ya simu kuhusu huyo teja Polisi watajua hata location ya huyo mtu muda fulani kulinganana mnara simu yake inaotumia kuwasiliana

Je Polisi wako tayari kwenda tayari kwenda far wa ajili ya laptop. La sivyo azima jina uitwe Komredi izengo Pinda au Komredi Mrisho Kikwete. Ndani ya siku tatu utapata kila kitu.



ndio polisi wetu
  • hawalipwi vizuri
  • wamekua wajasiriamali kwa kutumia kofia zao
  • myonge ndio hivyo anakoma
  • mwizi wako anajua kila unachofanya mkuu kuhusu mahangaiko yako
  • pesa inaonekana huna... kwasasa... negotiate na jamaa either umpe laki mbili unusu, au uwe unampa kwa mwezi (tena tumia huyohuyo polisi

HII NDIO SABABU WEZI WANACHOMWA MOTO
 
huyu jamaa kaja hapa kuomba msaada lakini hajapata bado msaada wowote kutoka kwetu ..i hope atajitokeza mtu mwenye uwezo wa kumsaidia..Polisi wetu ndio hao tena internet ni jambo la anasa sana
 
tafuta ela kama laki uigomboe hiyo mashine yako, ukijitia ujuaji ndo huipati tena..usisikize ushauri wa watu ambao wamekuwa overinfluenced kwa kuangalia csi sijui nini na matamthilia ya kubuni, polisi wa bongo wapok imaslahi zaidi, usije ukadhani wanapend kazi na fairness, na ustegemee watafanya kazi bila 'uwezeshaji',hata huko tigo kuna uezekano usifanikiwe lolote maana bongo 'uswahili' na incompetence ni ugonjwa wa kuambukiza. changamka dogo, huko ndo kugawana umaskini, next time utakuwa mwangalifu zaidi.
 
Mkuu hiyo laptop ni aina gan??
Kama ni TOSHIBA mpya mpya nistue kuna moja nimekutana nayo inapigwa biashara na mshikaji 1 hivi.
Contact zake zote mpaka mahome kwake.
 
Back
Top Bottom