mkuu nishai elewa sasa hivi ila kwa faida ya wote ngoja nifupishe maana yake hapa.
GDP interms of PPP (purchasing power parity) inatumika pale ambao unataka kulinganisha uchumi wa nchi tofauti. kwanza kabla sijaelezea GDP at PPP naomba nielezee namna ya kulinganisha uchumi wa nchi tofauti kwa kutumia exhange rates.
GDP at exchange rates ( kwa mfano uchukue pato la taifa la Tanzania kisha uli convert kwenda kwenye US Dollars, alafu uchukue nchi unayotaka kulinganisha nayo, labda tuseme Kenya, kisha uchukue pato la taifa la kenya nalo uli convert kwenda US Dollars.. alafu unalinganisha uchumi upi mkubwa kati ya Tz na Kenya maana GDP za nchi zote mbili tayari umeziweka kwenye common currency ambayo ni US Dollars)
tatizo kubwa linalojitokeza wakati unalinganisha uchumi wa nchi tofauti kwa kutumia GDP at exchange rates ni kwamba bei ya bidhaa baina ya nchi hizo mbili huwa ni tofauti. yaani kwa mfano Tanzania chungwa linauzwa
Tshs 200. wakati kenya chungwa hilo hilo linauzwa
Kshs 30. ambayo ni sawa na Tshs 600. Kwa hiyo mtu akiwa kenya na Tshs 600 anapata chungwa 1 tu, ila akiwa tanzania anapata machungwa 3.
hapa ndio ambapo ulipo udhaifu wa kulinganisha chumi za nchi mbili kwa kutumia
GDP at exchange rates. maana haitakupa uhalisia mzuri.
Kama tujuavyo pato la taifa ni jumla ya thamani ya bidhaa na huduma zilizo zalishwa ndani ya nchi katika muda maalumu ( haswa mwaka mmoja).
Ngoja nirahisishe mahesabu ili tuwe pamoja, Tu assume kuwa Kenya na Tanzania ndani ya mwaka 2017 wamezalisha machungwa tu. (turahishe mahesabu)
Tanzania imezalishwa machungwa
80, na kenya imezalishwa machungwa
40.
Hivyo basi
pato la taifa la Tanzania kwa mwaka 2017 litakua ( machungwa 80 @ Tshs 200 .. =
Tshs 16,000.
Na
pato la taifa la Kenya litakua ( machungwa 40 @Kshs 30 ..
Kshs 1,200.
Exchange rate 1 Kshs = 20 Tshs.
Hivyo basi Kshs 1,200 = Tshs 24,000.
kwa hiyo:
- GDP ya Tanzania = Tshs 16,000.
- GDP ya Kenya = Tshs 24,000.
Sasa hapo Ukilinganisha utaona Pato la taifa la Kenya ni kubwa kuliko Tanzania. ila kiuhalisia Tanzania ilizalisha zaidi ya kenya ndani ya mwaka huo 2017. Actually ilizalisha mara mbili ya ilichozalisha Kenya. hapa ndipo GDP (PPP) inapokuja kutatua mzozo kwani inatilia maanani utofauti wa bei za bidhaa baina ya nchi hizo.