Invigilator
JF-Expert Member
- Aug 16, 2016
- 3,207
- 5,990
Wakuu Salaam,
Ndugu zangu ni mwezi wa tano sasa tangu ndugu yangu (Me) amepata tatizo la afya la kupooza kuanzia maeneo ya kiunoni hadi miguuni.
Kiuno na miguu haifanyi kazi kabisa, hawezi kufanya chochote bila kupata usaidizi,kama familia tunaumia sana maana ni kijana mdogo (20s).
Tumejaribu kutafuta tiba Muhimbili imeshindikana, vipimo vikubwa vimefanyika lakini hakuna majibu ya kuridhisha juu ya hatima ya afya yake.
Nilikuwa nawaomba,ikiwa kuna mtu ana ufahamu juu ya tiba ya tatizo hili,au ikiwa kuna mtu anamjua mtu yeyote anayetibu matatizo ya kupooza atusaidie, sisi kama wana familia inatuumiza sana.
Natanguliza shukrani, karibuni kwa ushauri na maoni.