Msaada: Nawasha kila nikitoka kuoga

pole sana kwa tatizo so nakushauri ubadilishe maji unayo tumia ikiwezekata hata kuchemsha
 
pole. kuna kipindi nilikuwa na tatizo hilo kiasi kwamba ukifika muda wa kuoga naingia na kutoka. hakuna daktari aliyeweza kunisaidia. Tatizo lilikuja kupungua nilipohama arusha kwenda dodoma kisha dar. siku hizi mara moja moja nawashwa mapajani na miguuni. Kuna gazeti la mwananchi la wiki 2 zilizopita liliandika kwa kina sana kuhusu hili tatizo. Linasababishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na

-mzio wa kemikali fulani kwenye maji
- kuwa na ngozi kavu sana
- kuogea maji ya moto sana
- kuoga /kukaa kwenye maji kwa muda mrefu - hii huwa tunashawishika hasa wakati wa joto
- kujisugua

sayansi yake ya kutanuka na kusinyaa kwa ngozi sikuishika vizuri kutokana na ubongo wangu wa ndezi. Jaribu ku-google unaweza kupata majibu sahihi kulingana na hali yako. Inabidi uchunguze ni wakati gani unawashwa zaidi - asubuhi, mchana? sabuni je? maji ya halijoto gani? n.k
 
pole. mimi pia nilikuwa nawashwa mwili mzima hasa kipindi cha utoto na usichana. hakuna daktari wa ngozi aliyeweza kunisaidia na wengine walisema hawajawahi kuskia kitu kama hicho. nilipohama huko kaskazini na kuishi dodoma na dar ile hali ilipungua. siku hizi nawashwa mara chache na huwa ni miguuni.

Gazeti la mwananchi kama wiki 2 zilizopita walitoa makala ya afya inayohusu hili tatizo kwa kina sana. Unaweza kuwatafuta wakuelekeze daktari husika. Lakini baadhi ya mambo aliyoandika ni pamoja na

- kuwa na mzio na kemikali fulani kwenye maji au sabuni
-kutanuka kwa ngozi kunakoathiriwa na kukaa kwenye maji muda mrefu, kuogea maji ya moto sana au baridi sana, au kubadili joto ghafla. mfano unatoka kwenye mazoezi, bado mwili unachemka we unaenda kuoga maji baridi.
- kujisugua
- kuwa na ngozi kavu sana n.k

nakushauri u-google unaweza kupata maelekezo kulingana na hali yako kwani sababu ni nyingi sana na kutatua inabidi uanze kujaribu kila sababu mpaka ujue inayokuhusu. Kwa mfano mimi nilishajua nikiogea maji ya moto sana (huwa nayaita maji matamu) najua nitawashwa. Nikiwa mikoa ya baridi huko naoga kwa mbinde. sithubutu kujaribu maji ya baridi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom