Msaada: Nataka kupunguza kitambi

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
Wakuu,

Nina kitambi kinanikera sana, nimeshajaribu mbinu kibao za kukitoa, nimefanya tizi sana, nimebeba nondo, nimejinyima kula, lakini wapi ndo kwanza kinaongezeka, jamani kama kuna mwenye mbinu ya kupunguza vitambi anisaidie hapa.
 
Pole sana Mkuu... Ingia play store download application moja inaitwa egg diet itumie hiyo itakusaidia sana
 
Wakuu,

Nina kitambi kinanikera sana, nimeshajaribu mbinu kibao za kukitoa, nimefanya tizi sana, nimebeba nondo, nimejinyima kula, lakini wapi ndo kwanza kinaongezeka, jamani kama kuna mwenye mbinu ya kupunguza vitambi anisaidie hapa.

Shabikia SIMBA SC kitamb kitaisha mara moja
 
Pia download hapo hapo play store kitu kinaitwa "30 days ab challenge" itakusaidia sana.... Ukikwama nijuze
 
Wakuu,

Nina kitambi kinanikera sana, nimeshajaribu mbinu kibao za kukitoa, nimefanya tizi sana, nimebeba nondo, nimejinyima kula, lakini wapi ndo kwanza kinaongezeka, jamani kama kuna mwenye mbinu ya kupunguza vitambi anisaidie hapa.
Dawa ya kupunguza kitambi mimi ninayo ukitaka wasiliana mimi kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 
chakula! chakula! chakula ! jamani kitambi hakiwezi tuu kuja kama unazingatia ulaji bora kuna watu hawafanyi mazoezi lakini hawana vitambi
Ushauri bora kaka yangu ni angalia ulaji wako punguza kula wanga, punguza kula vyakula vye mafuta mengi, kama ni mnywaji wa bia punguza na misoda soda acha nayo maana haina umuhimu wowote mwili
Zingatia muda wa kula asubuhi ,mchana na hasa jioni .Epuka kula chakula kingi au kizito na kwakuchelewa usiku .
 
1. GET SERIOUS
2. EAT LESS EXERCISE MORE
Hizo ni mbinu mbili zilizoniondolea kitambi na kupunguza suruali toka size 38 mpaka 32, uzito toka kg 82 mpaka 70. huitaji kuingia gharama za madawa wala gym.
 
ID yako, mada zako na una kitambi inawezekana pia ukawa mfupi.. I can only imagine
 
Ushauri huu pia umewasaidia wengi: Fanya mazoezi ya kutumia vifaa vya ceragem. Kwanza kuna machine ya Ceragem na piakuna Low Frequency Stimulator - Slim Belt zote ni products za Ceragem zitakusaidia pasipo shaka. Ili mradi unazingatia nidhamu ya ulaji. Katika ulimwengu wa mwili, kitambi ni dampo la uchafu ambao unalundikana ukingojea kutolewa nje ya mwili. Ukiachwa bila kutolewa tegemea BP, kisukari, ugonjwa wa moyo, cancer na mengine mengi. Ceragem wapo Dar, Arusha, Mwanza, Dodoma au ni pm nitakuelekeza.
 
Ni rahisi sana, zingatia yafuatayo mpaka ktambi ktakapo isha.
1: Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na wanga mwingi
2: Fanya mazoezi zaid ya unayofanya, ila maintain chakula, namanisha portion ya chakula unachokula.
3: Jitahidi matunda na mbogamboga ziwe ni sehemu kubwa ya mlo wako.
4: Fanya mazoezi seriously, not once inabidi yawe sehemu ya maisha yako. Kila la kheri
 
Back
Top Bottom