Msaada nataka kununua pikipiki

Mastabenja

Member
Mar 23, 2012
25
6
ni ukweli usiopingika jf unapata taarifa sahihi za kila kitu pale unapohitaji.nimekuja jukwaa hili 5 tech ili nipate abc nataka kununua pikipiki iliyotumika.ni zile honda nyekundu zenye kikapu mbele sijajua brand name yake lakini nadhani ni cc 90.mimi nipo mkoani Ntazipata maeneo gani dar na bei zake inarange kiasi gani
 
Zipo dar kama uyoga. Bei yake ipo juu. Zinakula mafuta kidogo sana na ni imara. Tatizo spea na mafundi wetu wao wamezoea kutengeneza za mchina izo hawawezi sana. Mimi ninayo najuta kuinunua. Kama unatembelea wewe nunua mchina tu spea nyingi na bei poa mafundi wamezizoea
 
ni ukweli usiopingika jf unapata taarifa sahihi za kila kitu pale unapohitaji.nimekuja jukwaa hili 5 tech ili nipate abc nataka kununua pikipiki iliyotumika.ni zile honda nyekundu zenye kikapu mbele sijajua brand name yake lakini nadhani ni cc 90.mimi nipo mkoani Ntazipata maeneo gani dar na bei zake inarange kiasi gani

hapa umenimix kidogo kamanda.......hebu rudi tena......
 
Nilikuwa namaanisha model type brand name nimeshataja hata prof huwa anakosea.haukumbuki daktari alimfanyia mtu op kichwani badala yd mguuni
 
Ni honda ct 90 or yamaha t90t mate. Ni nzuri na imara,kuhusu matengenezo vifaa vinapatika sema tatizo kuwa bei yake vinakuwa juu sana maana ni genwn. Bei honda ni 1.8m,yamaha ni 1.6m. Ni ngumu balaa.mi ninayo yamaha,ni nzuri sna kwa shuguli za kilimo or shamba,fundi utakuwa unakutana naye kwenye servie ndogondogo tu kama kubadilisha oil.mchina sikushauri ni bora ununue boxer au bajaj nazo ni nzuri,japo boxer huwa zinasumbua engine.
 
mi nakushauri tafuta honda 110 km upo mikoani, inabeba mizigo balaa km ww ni mjasiriamali itakufaa, inuwezo wa kubeba kret 5 za bia, ina roho ngumu haifi ovyo.
hata hivyo vifaa vyingi vinaingiliana na mchina
 
daah! kama ina roho sasa hiyo tena haifai
 
Hata mimi natafuta kama hii hapa:

$(KGrHqF,!rYE88g6V!BoBPgdCZswV!~~60_14.JPG
 
Back
Top Bottom