Msaada; Nataka kufungua kampuni ndogo! mawazo tafadhali

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,800
6,294
Habari wakuu, nimepata wazo la kuanzisha kampuni ndogo itayokua inajishughurisha na kazi za rangi Tu, kupaka rangi kwenye Majengo, Nyumba za Makazi ya watu n.k, Na hiyo Ni kuanzia Wall painting, Floor painting (Epoxy metallic floor) n.k, nikiri kuwa idea hii ya kuanzisha kampuni ndogo imezaliwa kupitia bandiko hilo hapo chino.....
Ijue Epoxy Metallic floor, style ya kisasa ya floor!

Ambapo nilipokea simu nyingi Sana toka kwa watu wa kawaida hadi Makampuni makubwa ya ujenzi, but makampuni haya ya ujenzi karibia wote walinishauri niwe na kampuni hata ikiwa sio ukubwa Ila itakua rahisi kufanya nayo kazi, pia itakua rahisi hata kuomba kazi sehemu nyingine, kuliko Nikisimama Mimi kama Mimi.

Hivyo basi kampuni yangu itakua inajishughurisha na kazi zote za rangi Pamoja na Ku repair! Najua kuna wataalam hapa, kwana nataka kujua kwa aina ya kazi nnazotaka kufanya Je! Kampuni yangu itakua inatambulikaje? Kama kampuni ya Ujenzi ama? Pili, sina mbia kwenye wazo la kampuni hii, nataka nilisimamishe mwenyewe, Je! Ni lazima kampuni kama yangu iwe na Engineer? Na Engineer huyu Ni Hawa Hawa wa ujenzi ama? Tatu..... Unahitajika kuwa na kiwango flani cha pesa (Capital) kuwa na kampuni kama nnayoifikilia Nje ya gharama za usajiri wa Kampuni?

Mwisho....Kwa aina ya kampuni nnayotaka kuifungua, gharama zinaweza kufika kiasi gani in general? (makadilio)

NB:
Kama unacha ziada na unahisi Ni msaada kwangu, karibu!
 
Mkuu hapo waweza kufungua labour works specialized in Repair and paintings Class 1 ama fungua class 7 building works.........
 
Mkuu hapo waweza kufungua labour works specialized in Repair and paintings Class 1 ama fungua class 7 building works.........
Asante mkuu! Nimependa mchango wako, hivi ndo vitu ambavyo nlikua na nasubiri.... Kuna utofauti gani Kati ya class 1 na class 7?
 
Hiyo class 1 ni specialist labour based contractor unaspecialize na aina moja ya service compared to Class 7 ambayo unakuwa na wigo mpana kidogo......mkuu nicheki kuna kitu twaweza Fanya pamoja
 
Hiyo class 1 ni specialist labour based contractor unaspecialize na aina moja ya service compared to Class 7 ambayo unakuwa na wigo mpana kidogo......mkuu nicheki kuna kitu twaweza Fanya pamoja
Ok, basi nadhani hiyo class 7 inaweza kuwa poa zaidi coz nafikilia pia kufanya vitu vitu vingine kama kutengeza Ma Swimming pool n.k....ngoja nikucheki inbox mkuu tuongee!
 
Back
Top Bottom