Msaada: Nataka kudukua mawasiliano ya mke wangu

Msaada: Nataka kudukua mawasiliano ya mke wangu

Habari wanaBodi,

Kama nilivyotangulia kusema.

Nina mke ambaye tumekuwa naye katika ndoa miaka minne sasa lakini miaka ya karibuni nimeanza kupata mashaka na nyendo/tabia zake.

Mara kwa mara huwa napata safari nje ya mkoa hivyo muda mwingi tunakuwa hatupo karibu. Nimewahi kusikia kwa marafiki zangu wa karibu kuhusiana na tabia zake za kuchepuka kila ninapokuwa nimesafiri.

Nimejaribu kupeleleza lakini nimekosa ushahidi wa moja kwa moja maana naogopa kukurupuka nikakuta nimemkosea ama nimetoa hukumu kimakosa.

Kama kweli hiyo tabia anayo basi naamini kupitia mawasiliano yake naweza kupata hakika ili nifanye maamuzi sahihi ya kuinusuru ndoa yangu.

Wakuu naombeni kujua namna ya kufahamu kweli ya hili kwa namna yoyote ile ila kupitia udukuzi itafanya kazi vizuri zaidi naamini.

Naombeni muongozo wenu na hata kama kuna mfanyakazi wa mtandao wa simu huku aweze kunipatia msaada, nitatunza siri na reward itakuwepo kama ataweza kunifanikishia hili.

Natanguliza shukrani wakuu.
Ndoa ina miaka minne halafu unasema miaka ya hivi karibuni, mi naona miaka hiyo yote ni ya karibuni
 
Comment za wachache zinaonyesha kusaidia, wengi eti aache, kwanini aache??????? Mnamaanisha ni kweli anachepuka na mnaona ni sawa jamaa aendelee kuwa naye katika hiyo hali, hivi mkojeeeee??????


We mtaka ushauri, Go ahead na uchunguzi wako. Ila unapoamua kufanya jambo hili uwe mwangalifu kupitiliza, uwe tayari kwa matokeo utakayoyapata. Yafuatayo ni baadhi tu ya vitu utakavyokutana navyo.

1. Sms nyingi zenye dia, mpenzi, swty, wangu n.k wengi wanaweza kuwa wanawake wenzake. Sasa siyo inaingia sms moja usharuka juu utaumbuka mbele ya jamii na ndo pale kauli ya moja aliyesema inawezekana unazidiwa akili itakapodhihirika.

2. Wanaume wa jirani, anaofanya kazi, marafiki wa kawaida ambao huwa hatukomi kusifia wanawake maana tunaamini ndo jinsi wanajisikia vzr, sasa ukiona tu 'ulipendeza sana dear' , tulia usikurupuke maana wengi wao huwa wanamshawishi kisirisiri ingawa wanazugwa kujibiwa majibu flani neutral. Usiogope hawatafanikiwa, mwache awe huru kutaniana na wenzake.

3. Unajua huyo mkeo alikuwa na ex (s), sasa wengine wanakuwaga siyo wastaarabu. Ukute wanamdai picha zake za siku hizi, wanapiga story za kipindi kile, mwingine atakuwa anadai kupasha kiporo. Na mengine mengi ya namna hiyo.

4. Ukikuta kweli kuna mawasiliano serious na yanayogusa ile contract yenu halisi sasa hapo ndo utulie ufuatilie kwa karibu hadi ujiridhishe kama ni kweli analalwa, na kweli kabisa una ushahidi wa hilo. Hapo sasa usiangalie nyuma.

Embu anza na hayo nitarudi tuendelee
 
Back
Top Bottom