WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,415
- 1,379
Wakuu,nina shamba la familia la ekari 4 lenye hati ya kimila tuliyopewa 2010 mwezi wa saba.
Kulingana na hali ya kiuchumi ya sasa,ninataka niunganishe familia yangu yenye watu wazima 6 km kikundi cha familia,tuandae business plan,katiba na tuweze kwenda bank kuomba mkopo wa shilingi miliini 20.
Nina malengo yafuatayo,baada ya kupata mkopo,
1.Kuchimba kisima cha kina kirefu
2.Kununua pamp ya maji
3.Kufunga drip irrigation system
4.Kuanza kilimo hai (organic farming) cha umwagiliaji,mazao ni
-mboga mboga
-nyanya
-Vitunguu nk
Pia tutalima chakula ikiwemo mahindi,mtama nk
Bila kusahau maharage na mazao jamii ya kunde.
Mimi ni mhitimu kutoka SUA na nilikua nafanya kazi kwenye shirika binafsi lakini naona naweza tumia fursa hii na naamini familia yangu nitaitoa,Familia yangu iko Bariadi,wilaya ya Itilima.
Bank nazowaza kupata mkopo ni CRDB na NMB kama mawazo yangu yatakubaliwa.
Kama nikipata huu mkopo,mie ni mtoto wa pili,nimeoa na kaka yangu pia kaoa,mdogo wetu wa kike naye kaolewa lakini waliachana na mme wake.
Katika familia kiwango cha elimu ni hivi
1.Baba na Mama ni la saba
2.Kaka na mke wake ni la saba
3.Mimi degree na mke wangu ni degree(mwalimu)
4.Mdogo wangu wa kike ni form 4
5.Mdogo wangu mwingine wa kike ni form four lakini amefaulu kujiunga kidato cha tano hapo badae mwezi wa saba kama sikosei.
6.Waliobaki ni wadogo wetu watatu bado ni under 18 so hawatakuwepo kwenye mambo ya kisheria lakini haki na gawiwo la kifamilia watakua wanapata hasa likielekezw8a katika gharama za shule na mahitaji yao muhimu.
Kwa kuwa kidogo mie nina uelewa wa juu kielimu,nataka niwe ndio Chief operating Manager wa familia,kuwangoza ndugu zangu na kusimamia operation zetu za familia.Baba yangu atakua mwenyekiti tu lakini atakua na maamuzi katika mikakati ya kufamilia na kuamua kesi ndogo ndogo za kufamilia punde zikitokea,lakini mambo ya biashara,kusimamia marejesho ya mkopo na uwajibikaji mie nitajitwika mzigo huu.Naamini baada ya miaka 5-10 nitakua nimemaliza kulipa mkopo na faida juu.
Naomba ushauri wa kisheria,kiuchumu,kijamii na kimawazo,je hili wazo langu linaweza likafanikiwa? Kma ndio nifanye nini ili nipate mkopo haraka? Kama hapana nirekebishe wapi ili nitimize lengo hili?
Kama wazo langu ni zuri naomba mnielekeze taratibu za kufauta nipate mkopo,lakini kabla ya hapo naomba mtu wakuniandalia project plan na business plan,nitahitaji pia mwanasheria wa kuniandalia katiba na partnership deed
Nitashukru sana,mimi ni mtaalam wa usindikaji wa mazao ya chakula km na wewe unahitaji kiwanda cha kusindika chakula cha binadam nitafute tu nikusaidie,nikuandalie kila kitu ikieemo kusajiriwa na taasisi za kiserikali TBS,TFDA,OSHA etc
Asanteni wakuu,pia unaweza ukanifuata PM kwa kunishauri zaidi