Msaada: Natafuta eneo lililotulia nje kidogo ya mji wa Dar kwaajili ya kupumzika

Posto Bella resort IPO Boko magengeni kwa mbele baada ya hisaje park unaingia ndani km 2km HV. Uko utatulia bila usumbufu wowote mkuu.
 
Ushuani hakuna mihemko ya Kwamtogole
kwa mtogole sikai hata kwa makofi,ukifua nguo inabidi ukae kuzilinda na ukienda kuoga mlango funga na kufuli,nimezoea maisha ya kuinjoi hapa vigwaza, nimeamini mtu kwao inaelekea unapapenda sana kwa mtogole au mahakama ya simu,
 
Habarini wakuu,
Natafuta eneo zuri ambalo liko nje ya mji wa dar ambapo hakuna kelele kwa ajili ya kukaa na kutuliza akili kwa kuangalia mazingira asilia. Nimekuwa nikifanya hivyo tangu nikiwa mkoa ila tangu nije dar nimekuwa nashindwa kupata eneo kama la aina kama nilivoeleza hapo juu. Kuna mtu niliongea nae majuzi akaniambia kuwa dar es salam zoo panafaa lakini mimi sikuwa na lengo la kwenda zoo. Je, nje ya dar zoo katika maeneo yake ya jirani kuna sehemu za kupumzika bila bugudha yoyote?
N.B. .maeneo hayo yasiwe fukwe au mazingira ya kutengenezwa na binadamu, yawe 90% natural.

Shukran
usipate shida njoo huku kwetu vigwaza kuna kila kitu maziwa,nyama pori,mihogo na matunda ndio usiseme karibu sana bwana mdogo,
 
kwa mtogole sikai hata kwa makofi,ukifua nguo inabidi ukae kuzilinda na ukienda kuoga mlango funga na kufuli,nimezoea maisha ya kuinjoi hapa vigwaza, nimeamini mtu kwao inaelekea unapapenda sana kwa mtogole au mahakama ya simu,
Khe nyinyi wenye nguo za kulinda mkifua huku kakumifai. Sisi huku tunaishi una khana pair moja, kitenge pair moja, dear moja. Mganga yako mtaa nzima wanaijua kwakua ni kauka nikuvae.

Tukienda Madale kwenye arobaini za watoto wa Diamond tunaazimana madera
 
kunawafaa nyi wenyewe,sisi huku tumezoea kuonana na jirani ni kama mita 200 na maswahiba wa karibu ni nyani na ngedere,bila kumsahau nguruwe pori,
 
Habarini wakuu,

Natafuta eneo zuri ambalo liko nje ya mji wa Dar ambapo hakuna kelele kwa ajili ya kukaa na kutuliza akili kwa kuangalia mazingira asilia.

Nimekuwa nikifanya hivyo tangu nikiwa mkoa ila tangu nije Dar nimekuwa nashindwa kupata eneo kama la aina kama nilivoeleza hapo juu.

Kuna mtu niliongea nae majuzi akaniambia kuwa Dar es Salam Zoo panafaa lakini mimi sikuwa na lengo la kwenda Zoo.

Je, nje ya Dar Zoo katika maeneo yake ya jirani kuna sehemu za kupumzika bila bugudha yoyote?

N.B Maeneo hayo yasiwe fukwe au mazingira ya kutengenezwa na binadamu, yawe 90% natural.

Shukrani
HAKUNA
 
Back
Top Bottom