Natumai wote u wazima wakuu. Kwanza ningependa kuwashukuru wote kwa michango yenu yenye burasa, mbarikiwe sana na muendelee na moyo wa kusaidiana.
Mimi ni kijana ambae nasoma form five kwa sasa na ninategemea kuspecialize kwenye mambo ya computer nifikapo chuo.
Ila hivi vitu viwili 'software engineering' na 'computer programming' huwa vinanichanganya na ninashindwa kujua tofauti yake maana huwa naona kama hivi vitu vyote vinahusu computer programs. Naomba msaada wenu wakuu nipate fahamu vema tofauti kati ya haya mambo mawili.
Natanguliza shukrani zangu kwenu na ninawatakia pasaka njema....
nikijaribu kukumbuka kwa haraka haraka,
Kwa kiswahili, Computer Programming; unaweza ukai-program computer bila kutengeneza software, nikiimanisha kwamba, unatumia programs zilizopo kuifanya kumpyuter ifanye unavyotaka.
Pia unaweza kuita computer programming, kama njia ya kuifanya computer ifanye unavyotaka kwa kutengeneza programs zako.
Inapokuja kwenye Software Engineering; hapa kuna vitu vingi sana vya kuangalia. kwa kifupi, ni namna ya kutengeneza software katika standards, njia (methodology) zinafahamika;
Yaani hauamki asubuhi na kuanza ku-program, hapana, isipokuwa unaanza kwenye upembuzi yakinifu (feasibility study), unakusanya mahitaji (software/system requirements), then unakuja kwenye design (hapa kunakuchagua tools kwa ajili ya ku-design pamoja na methodology), then unakuja kwenye coding, maintenace, n,k.n.k
kwa kifupi S.E ni pana sana ( hiyo computer programming inamezwa ndani)