Msaada: Naogopa kazi mpya

'Mboga ya majani penye mapendano Ni Bora kuliko ng'ombe mzima alienona penye magomvi'
 

Asante kwa ushauri wako
 
Kuna kazi nilikuwa nafanya awali nilikuwa naingia Kazini saa 2 asubuhi kutoka saa 10 Jioni. Mshahara kiduchu
Kuna kazi niliipata niliyotakiwa kuingia Kazini saa 1 asubuhi, kutoka saa 11 Jioni plus kuwekewa malengo na boss, Kila baada ya miezi 3 unatoa report na kufanyiwa tathmini, but mshahara ulikuwa almost mara 3 ya ule wa awali.

Nilichofanya ni kuji-twist kuendana nayo. Huwa najisemea, kama Kulala nitalala nikishafika miaka 60 huko nikistaafu.

Wakati huu wa Ujana ndiyo muda wa kujitesa ili kuhakikisha Tukizeeka hatuwasumbui watoto/ndugu kuombaomba hela za matumizi
 
Sawa ila nafasi zinapatikana so naumia kuziacha
Unahitaji ku grow na katika suala la kukua katika career lazima ukutane na changamoto mpya. Hayo mapungufu uliyonayo ilimradi umeshayajua utaweza kuyatatua.

Hilo pepo la kimasikini litoke kwa Jina la Yesu.
Nenda kaongeze CV na ufanye kazi kwa Bidii. Kuwa open minded katika kazi hiyo sehemu ambayo huelewei uliza wenye ujuzi watakusaidia.

Kila la kheri.
 
Usijitese sana ndugu yangu..haya maisha tunapita..si umeona wanaume wanaisha tu na kuwaacha akina mama/wake zao tu.
Stress take your time ku enjoy ili mradi haumkosei muumba wako.

mimi bhana ni mara 100 niwekeze effort kubwa sana kwenye kazi zangu kuliko kumtajirisha mtu..
Mtu unamwingizia millions of money kwa mwezi mtu akipewa 1M per month anaona katoboa.
 
Kwanza nikupongeze kwa kufanikiwa kupata ajira mpya, jitahidi sana kujikubali wewe ulivyo usiwe unajilinganisha na mfanyakazi yeyote ktk utendaji wako, mtangulize Mungu mbele siku zote, thubutu jisemeshe wewe unaweza na utaifanya hiyo kazi iliyopo mbele yako maana ukijiogopa hivyo basi mambo yako binafsi hutajiwekea malengo yoyote hata ungalipata kiasi gani cha fedha.
 
Safi
 
Mkuu naomba nisaidie kama kuna nafasi na mimi mkuu. Nipate mishe angalau nipate ugali mkuu. Natanguliza shukrani zangu.
 
Umesema sahihi Mkuu

Japo Waswahili wanasema Mtumikie Kafiri upate Mtaji wako.

Wakati unapambana kufanya kazi za watu, hakikisha una serve na kuanzisha biashara zako binafsi.

Ni jambo lisilo na Afya, ukipata shida hata ya milioni 3 inakushinda kuitatua hadi uanze kukopa Kwa watu.

Imagine ukishastaafu na hauna kipato endelevu si utakufa baada ya Mwaka mmoja
 
Nakuelewa sana mkuu

Kama unajijua hauna umakini jitahidi kila kazi inayotoka uifanye hapo hapo,hii itakusaidia kuihakiki mara nyingi uwezavyo...usisubiri deadline ndio uanze kukimbizana nayo

Jitahidi pia kusoma mambo yanayohusu hiko unachofanya
 
Huyu atakuw incompetent..

Mie kuna kazi niliwah fanya sikuw na kauli ya kusema kitu fulani sijui au sikifahamu. Napewa Task za senior officers ndio nifanye mimi Junior.

Nikitoka kazini natafuta watu wa taasisi zingine na kuingia ktk mitandao kuona hicho kitu kinafanyikaje exactly, then naunda sasa kile nachoona kinafaa.

Namshukuru Mungu, nilijua vi2 vingi nje ya level niliyokuw nayo, sasa hivi nimekuw mkongwe ingali umri ni mdg san ila kazi za Director nafanya vzr maana ndio yale niliyokuw natwishwa angali naanza kazi.

Kuwa flexible mtoto wa kiume
 
Endelea na kazi yako ya awali kama hujiamini na kama kuna probation miezi 9 ni hatari kwamba utakosa kazi zote na itakuwa majuto!
 
Hii kutongoza....imenikumbusha jamaa kashauriwa kumtongoza boss wake( mkurugenzi).... jamaa kweli baada ya kupambwa na wenzie akajitosa...kampa mama maneno....mama kaona duuh! Kijana pengine ana malaria kichwani...akamshauri rudi nyumbani kapumzike....wenzie wakazidi kumtia kichwa...ati mama keshakuelewa...wee nenda Katie kinywaji halafu mfuate nyumbani kwake........
Kwa kifupi imekuwa kama laana....mpaka leo jamaa anashinda kwenye mabanda ya wanzuki hakupata kazi tena....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ