Msaada namna ya kumlea mtoto kupenda shule

Msaada namna ya kumlea mtoto kupenda shule

mezakuu

Senior Member
Joined
Apr 19, 2016
Posts
156
Reaction score
131
Wakuu msaada, Nina wadogo zangu wawili mmoja yupo secondary anasoma boarding na mwingine yupo shule ya msingi.

Wa secondary huyu kashaamishwa shule nyingi sana tokea mdogo na sababu kubwa ni anafeli darasani nyumbani tumeshapiga hadi tumechoka, baba yeye ameshajitoa kumfatilia kabakia kulipa ada tu na anaomba tumsaidie kulea siwezi sema ana low iq maana ukimpa vitu kama computer na simu ni rahisi kwake kuendana navyo tokea mdogo.

Hajawahi kufundishwa gari ila siku alikuwa likizo kawasha kaondoka kwa ufupi vitu vya mtaani anavishika haraka.Wa shule ya msingi yupo vizuri ila yeye anaweza akaenda shule asiandike mara asimalize mtihani ana uvivu fulani japo anafaulu kwa kiasi chake ila bado anahitaji msaada maana hiyo tabia yake walimu tu wanalalamika kila mara.

moja ya vitu vinavyomuaribu mdogo wangu wa sekondari ni kwamba alipigwa sana kipindi mdogo sababu ya shule nahisi kashajiona hawezi na imemfanya kuwa muoga kupitiliza akiwa nyumbani.
 
Elimu anayopata haiendani na interest zake ndo maana, huyo anayependa magari mpelekeni hata veta huko atakutane na vitu vya interest yake.
Tatizo huwa ni mtu ana-interest na magari afu wahusika wanalazimisha afauru biology huko
 
Ni vizuri ukaa naye huyu wa sekondari na ukamfundisha kwa upole na nidhamu mwambie faida za elimu na pia hasara za kutokuwa na elimu, hakika kuna wakati mwanafunzi wa sekondari anakuwa anachukia shule kwa kiasi kikubwa lakini kadri anavyo zidi kusoma anakuwa anaipenda shule.

Ni vyema ukawa na muda wa kuwafundisha na hata kuwashawishi wapende shule wote wawili, na ukishamjua tabia za mwanafunzi basi ni vyema ukaendana naye lakini taratibu na mwisho ya yote ataipenda shule.

Mfano daktari bingwa wa upasuaji, dr. Ben Carson alikuwa hapendi shule na anafeli lakini mama yake aliweza kumtengenezea mazingira bora na hatimaye amekuwa daktari bingwa hakika sio jambo jepesi Bali ni kazi ngumu kushawishi.

Unaweza kuwalea wadogo zako wote kwa mfumo huu.

1. Wape muda wao wa kupumzika.

2. Wape muda wa kusoma ikiwemo usimamizi chini yao.

3. Ratiba pia ni muhimu kuwapa wakiwa nyumbani, mfano asubuhi hadi mchana wanakuwa wanafanya mambo mengine kama kazi, na alasiri saa 9, wanapumzika kama muda upo lakini hakikisha kila jioni lazima wasome masomo kadhaa kwa saa 1 au 2.

4. wape testi kila wiki au kila siku hii pia kumjenga kusoma vizuri.

5. Mpe moyo na uangalifu wala usimkatishe tamaa.


Hakika naamini watabadilika ukali haumsaidii mtu kufanya vizuri bali ni kumpa moyo na kuvutiwa zaidi na kile anacho ambiwa au kuona ( to be motivated )
 
Elimu anayopata haiendani na interest zake ndo maana, huyo anayependa magari mpelekeni hata veta huko atakutane na vitu vya interest yake.
Tatizo huwa ni mtu ana-interest na magari afu wahusika wanalazimisha afauru biology huko
mkuu ni kweli ila kuna knowledge ya form 4 ambayo ni muhimu inabidi afaulu huwezi kuwa fundi mzuri huji hesabu shulepia inasaidia mtu kuweza kufikiria zaidi
 
Wakuu msaada, Nina wadogo zangu wawili mmoja yupo secondary anasoma boarding na mwingine yupo shule ya msingi.

Wa secondary huyu kashaamishwa shule nyingi sana tokea mdogo na sababu kubwa ni anafeli darasani nyumbani tumeshapiga hadi tumechoka, baba yeye ameshajitoa kumfatilia kabakia kulipa ada tu na anaomba tumsaidie kulea siwezi sema ana low iq maana ukimpa vitu kama computer na simu ni rahisi kwake kuendana navyo tokea mdogo.

Hajawahi kufundishwa gari ila siku alikuwa likizo kawasha kaondoka kwa ufupi vitu vya mtaani anavishika haraka.Wa shule ya msingi yupo vizuri ila yeye anaweza akaenda shule asiandike mara asimalize mtihani ana uvivu fulani japo anafaulu kwa kiasi chake ila bado anahitaji msaada maana hiyo tabia yake walimu tu wanalalamika kila mara.

moja ya vitu vinavyomuaribu mdogo wangu wa sekondari ni kwamba alipigwa sana kipindi mdogo sababu ya shule nahisi kashajiona hawezi na imemfanya kuwa muoga kupitiliza akiwa nyumbani.
Wapeleke kashikashi group hamna shule hapo.
 
mkuu ni kweli ila kuna knowledge ya form 4 ambayo ni muhimu inabidi afaulu huwezi kuwa fundi mzuri huji hesabu shulepia inasaidia mtu kuweza kufikiria zaidi
Watu husema hvyo, hiyo hupelekea kulazimisha mtu asome na mwisho wake huwa ni kuferi hiyo form 4.

Elimu ya msingi ni elimu mama, akiipata hiyo acha apambane na interest yake ktk interest akiona anahitaj kujua zaidi hesabu namna itatafutwa atajifunza hiyo hesabu
 
dogo atakuwa amejitambua maada akimcheki prof ..... mambo anayoyafanya anaona bora aache shule
 
Back
Top Bottom