Msaada: Nahitaji kufika Leaders Club, niko Makumbusho stand DSM

Msaada: Nahitaji kufika Leaders Club, niko Makumbusho stand DSM

Status
Not open for further replies.

mafuru

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2014
Posts
379
Reaction score
38
Jamani naombeni ramani ya kuniwezesha kufika Leaders Club now.

Niko makumbusho stand hapa DSM na nahitaji kufika viwanja vya leaders club DSM.
 
Panda daladala ya makumbusho/posta au makumbusho/stesheni shuka makaburuni chukua boda boda au bajaji hapo makaburi ya kino umefika
 
Broo maelezo yako ni magumu sana
Sijakuelewa mkuu
Nielekeze vyema hapo ntapotea kabisa mkuu nisikufiche
Me ndo kwanza nimefika dar
 
Mkuu nimwambie konda anishushe makaburi ya wapi please
Na nikishashuka hapo makaburini napanda bajaj naelekea kinondoni ama
Mbona sijakusoma mkuu?
 
Broo maelezo yako ni magumu sana
Sijakuelewa mkuu
Nielekeze vyema hapo ntapotea kabisa mkuu nisikufiche
Me ndo kwanza nimefika dar

We panda gari za makumbusho stesheni mwambie akushushe makaburini kinondoni ukishuka hapo uliza tu leaders umefika
 
Makumbusho stesheni mbona naulizia sizioni wananambia ni chache kwa hiyo kwa sasa hazipo
Nipe plan b mkuu
 
Broo maelezo yako ni magumu sana
Sijakuelewa mkuu
Nielekeze vyema hapo ntapotea kabisa mkuu nisikufiche
Me ndo kwanza nimefika dar
Utapoteaje mchana mkuu wangu tena Bongo tu hapa je siku ukitakiwa ufike china kijijin huko itakuwaje...Mi nadhani bodaboda zimerahisisha sana maisha kamata jamaa wa bodaboda mchimbe mkwara kwamba we njoo hapa unapajua Leader club....Shilingi ngap oooh elfu tano ..unachimba biti tena aha twende ntakupata buku 4...Yaan argument yako iwe kwenye bei tu usimuonyeshe huyo jamaa kuwa wewe ni mgeni...Simple utajikuta Leader ama kama si mpenzi wa bodaboda kamata Tax kwa style hiyo...All the best
 
Jamani naombeni ramani ya kuniwezesha kufika leaders club now
Tafadhali wanajf naombeni msaada wenu wa hali na MALI Niko makumbusho stand hapa DSM na nahitaji fika viwanja vya leaders club DSM

Sory we ni justin mafuru?
 
Makumbusho stesheni mbona naulizia sizioni wananambia ni chache kwa hiyo kwa sasa hazipo
Nipe plan b mkuu

panda za posta shuka mbuyuni then chukua boda boda mwambie unaenda leaders club watakuchaji buku utafika au chukua boda waambie unaenda leaders kutoka makumbusha hadi hapo nadhani ni buku 2000 au tatu kwa kisingizio cha dola imepanda
 
Unavuka kituo cha mbuyuni hapo njia panda ya leaders au ni kabla ya mbuyuni mkuu
 
Unavuka mbuyuni, bt ni vizuri ukashuka mbuyuni ukachukua boda cz pale njiapanda hakuna kituo
 
hahaha wewe jamaa kweli kiazii.
ila woga wako ndio kupotea kwako na kushindwa kwako unakokwenda.

yaani upo makumbusho stend harafu unauliza jf?? ww kweli huna shida hapo kuna wapiga debe na makondakta wangapi?? muulize konda unataka kufika leder club je unapanda daladala ya wapi?? atakwambia na sehem ya kushuka mkuu.

au akikwambia kuwa ni daladala ya posta wewe panda ukiingia tuu mwambie konda au kaa karibia na mlangoni mwambie konda kuwa unaenda leder club atakushusha kituo husika .ukisha shuka usiwe na wenge mfuate boda boda mwambie unataka kufika leders club sh ngapi atakupa bei yake hapo sasa akili kumkichwa kama utakubaliana naye au utamshusha bei lakini kama kawa ubishi mhimu hata akikwambia elfu 2000 ww unamwambia una buku.

dar mchana huu kama unapesa mkononi huwezi potea bana sehem maarufu kama hiyo yaani hapo hapo ulipo makumbusho kama una hera ya kutosha chukua boda boda au bajaji mwambie akupeleke leders club
 
Unavuka kituo cha mbuyuni hapo njia panda ya leaders au ni kabla ya mbuyuni mkuu

Baada ya mbuyuni ukishuka kilima then unaingia kulia. Natumaini umefika, kumbuka kutojionyesha kuwa haulijui jiji.
 
panda daladala ya makumbusho posta. shuka kituo kinaitwa CONTAINER/DSTV. vuka upande wa pili wa br ya ali hassan mwinyi utaona barabara ya lami inaitwa TUNISIA RD.

pandisha na TUNISIA RD kama mita 150 hivi utaona kona ya kwanza kushoto inaitwa DAHOMEY RD ingia na hio barabara Leader Club ni geti la kwanza kulia.

karibu napata supu sasa hivi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom