Msaada: nahitaji honi za mlio mkali

Tisha-TOTO

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2010
Posts
1,175
Reaction score
604
Wakuu. Seriously mwenzenu nahitaji kununua zile honi zenye mlio mkali sana, huwaga nazisikiaga sanasana kwenye magari makubwa au hata zile zitumikazo kwenye garimoshi (treni).

Wapi zinauzwa hizi vitu kwa hapa Tanzania (preferably Dar)?? Hata za mtumba poa tu...
 
Kwa ajili ya gari? Gari aina gani? Lori au gari ndogo?
 
Gari kubwa zinatumia honi za upepo (zile honi kali), gari ndogo nyingi hazitumii mfumo wa upepo kwenye honi. Swali bado liko vile vile, unahitaji kwa ajili ya mfumo wa upepo ama wa umeme ( mfumo wa umeme honi zake siyo kali kama mfumo wa upepo)
 
In that case, nitahitaji hiyo ya upepo. Nitaipataje mkuu??
 
wataka jambisha watu wewe!

Mkuu, tuacheni utani.....mwenzenu ninahitaji haya mavitu kiukweli. Kama unajua nitakapoweza kuzipata please saidia.

Unaweza kuni-invoice hii huduma ya kunifahamisha tu sehemu ya kupata hii bidhaa. Am serious.
 
Unafunga kwenye gari gani mkuu, kama ni fuso, eicher kama za uda sawa but saloon and station wagon itabidi ununue na mfumo wa upepo ili iweze fanya kazi.0754490309 huyu ni fundi yupo gerezani kariakoo na maduka yapo hukohuko waweza mcheki
 
Nenda maduka yanayouza vifaa vya magari makubwa kama scania au FAW utapata
 
Ivi kwanini hakunaga digitali ya honi!!!! si wangeweka honi mpya mfano, honi ya kubweka kwa mbwa, ama mngurumo wa simba, watu watakua wanapata attention haraka, honi za kawaida tumezoea.
 
Unafunga kwenye gari gani mkuu, kama ni fuso, eicher kama za uda sawa but saloon and station wagon itabidi ununue na mfumo wa upepo ili iweze fanya kazi.0754490309 huyu ni fundi yupo gerezani kariakoo na maduka yapo hukohuko waweza mcheki
Asante mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…