Msaada na Ushauri: Biashara gani sio risky kati ya duka la pembejeo na pharmacy?

Aunt Catherine

New Member
Jan 8, 2021
4
20
Ndugu zangu naomba ushauri wa biashara ipi Haina risky sana kati ya hizo mbili (pembejeo na pharmacy) nmemalza chuo na mtaji kama wa million tatu napenda kufanya biashara ya pharmacy au duka la pembejeo lakini elimu yangu ni engineering kwa maana hiyo sipo vzur Sana na elimu ya hvo vtu viwili, samahani kwa mwenye ujuzi wa pharmacy au pembejeo naomba msaada wa kibiashara hizo ili nipate mwanga kwa faida na hasara zake.

Nipo Mbeya
 
andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,728
2,000
Risk ni nini katika biashara? Hakuna biashara ambayo haina risk-Katika maisha hakuna kitu ambacho hakina Risk kwani kila jambo ulifanyalo huwa ni TRADEOFF ya rasilimali muda, pesa, akili n.k.

Unapoamua kufanya biashara zingatia kwamba kila biashara ina changamot zake.Swali la kujiuliza je unafahamu utaratibu na mahitaji kwa biashara hizo zote? Kwa mfano mahitaji ya leseni. Je, unafahamu bidhaa ambazo zinatoka sana katika biashara ya aina unayotaka?Je umeshapata eneo? Je, unafahamu jinsi ya kuendesha aina hii ya biashara?

Ni kitu gani kimekufanya uchague kufanya aina hii ya biashara na sio aina nyingine?Hayo ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa kujiuliza wakati wowote unapotaka kufanya biashara kisha baada ya kujiuliza na kutafuta majibu yote unaweza kuamua iwapo unaweza na uko tayari kufanya biashara.

Ushauri wangu tafuta mtu unayemfahamu anafanya moja ya biashara hizo zungumza naye na umuulize maswali sahihi ili akupe majibu sahihi then uamue iwapo ni aina ya biashara unayoweza kufanya kwa kutegemea kiwango cha mtaji na eneo ulipo. Kwa msaada zaidi DM
 
Aunt Catherine

New Member
Jan 8, 2021
4
20
Risk ni nini katika biashara?Hakuna biashara ambayo haina risk-Katika maisha hakuna kitu ambacho hakina Risk kwani kila jambo ulifanyalo huwa ni TRADEOFF ya rasilimali muda,pesa,akili n.k.

Unapoamua kufanya biashara zingatia kwamba kila biashara ina changamot zake.Swali la kujiuliza je unafahamu utaratibu na mahitaji kwa biashara hizo zote?Kwa mfano mahitaji ya leseni,Je unafahamu bidhaa ambazo zinatoka sana katika biashara ya aina unayotaka?Je umeshapata eneo?Je unafahamu jinsi ya kuendesha aina hii ya biashara?

Ni kitu gani kimekufanya uchague kufanya aina hii ya biashara na sio aina nyingine?Hayo ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa kujiuliza wakati wowote unapotaka kufanya biashara kisha baada ya kujiuliza na kutafuta majibu yote unaweza kuamua iwapo unaweza na uko tayari kufanya biashara.

Ushauri wangu tafuta mtu unayemfahamu anafanya moja ya biashara hizo zungumza naye na umuulize maswali sahihi ili akupe majibu sahihi then uamue iwapo ni aina ya biashara unayoweza kufanya kwa kutegemea kiwango cha mtaji na eneo ulipo.Kwa msaada zaidi DM
Ubarikiwe Sanaa nduguyngu umeniongezea kitu kichwani
 
Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,493
2,000
Sema duka la dawa na sio phamacy ni vitu viwili tofauti kwa uzoefu hiyo 3m haitoshi chochote duka la dawa angalau 5m garama kubwa ipo kwenye maintainance ya chumba kutengeneza display cases inaweza kuwa 2m+ mfano alluminium case ya 6ft by 6ft upana wa 33cm each 900k counter urefu 3ft upana 6ft inaweza kuwa 400k uweke 2 za pembeni 500k ufanye partition ya stoo utatumia ceiling board 2 mbao 2 by 4 kama 6 zipasuliwe kuwa 12 mbao 2 pana na fundi total kama 200k. Mlango wa alluminium kulingana na mlango minimum 600k, feni 80k kameza 120k viti 2 muuzaji na mteja 30k. Mtaji wa dawa 2M inatosha.

Uonane na bibi afya wa eneo na mphamasia wa wilaya kwa ukaguzi utalipia kibali 100k ama 50k lesseni ni 100k TRA Wakukadirie mapato.... ukipata muuzaji mujanja anakuja na dawa zake, hii biashara inamambo mengi mpaka nakuonea huruma mwanzo ni mgumu ukipata wrong medical dispenser.

Kwa phamacy ya rejareja 15-20m zinaweza kutosha kuanzia mambo ni mengi uwaone na wahusika kupata abc zingine natumai nimekupa ka mwanga fulani. Ukiweza kununua materials mwenyewe kisha ukamlipa tu ufundi itapunguza garama ukienda vibaya ata 4m haitoshi kutengeneza chumba cha duka la dawa.
 
Ahsante Sana nduguyngu
 
Patroman

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
647
1,000
Lakini pia jaribu kupekua kidogo humu jamiiforum....mijadala kusuhu biashara hizo imeisha jadiliwa kwa kina na wadau mbali mbali.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
12,946
2,000
Pharmacy kwahiyo hela ni ndogo. Utahitaji kutengeneza chumba kwa standard zao na uajiri mfamasia na msaidizi wake. Utashangaa hiyo tatu imeishia kwenye matengenezo ya chumba tu.
 
kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,072
2,000
Risk namba moja, ni kutokuwa na uelewa wa hizo biashara, fanya biashara inayoendana na ulichosomea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom