Msaada: Mwenye ujuzi wa kuagiza gari, aina ya caldina

themagainst

Member
Feb 28, 2011
51
11
Heri ya mwaka mpya 2016.

Samahani msaada kwenye tuta, nina maswali machache;

1. Naomba kufahamu kuhusu magari aina ya Caldina uimara, gharama ya kuimudu, spare ,usalama, mafuta. n.k

2. Je kwa wenye uzoefu,gari hii nikiiagiza inauzwa dola 1400, ni ya mwaka 2007,ina cc 1790, imetembea km 120,000 na ipo kyushu je gharama mpaka kuitoa bandarini Dar es salaam na usafirishaji itakuwa kama shs ngapi?

Mwenye kujua mambo hayo anisaidie please ahsanteni, karibuni
 
Last edited by a moderator:
heri ya mwaka mpya 2016

samahani msaada kwenye tuta,nina maswali machache

1.Naomba kufahamu kuhusu magari aina ya Caldina...uimara,gharama ya kuimudu,spare,usalama,mafuta. n.k

2.Je kwa wenye uzoefu,gari hii nikiiagiza inauzwa dola 1400, ni ya mwaka 2007,ina cc 1790,imetembea km 120,000 na ipo kyushu.....je gharama mpaka kuitoa bandarini dar es salaam na usafirishaji itakuwa kama shs ngapi?

mwenye kujua mambo hayo anisaidie pls.....ahsanteni,karibuni
Caldina ni gari nzuri kwa maana ni jina la TOYOTA, ila zingatia mambo kadhaa kabla ya kununua gari; 1 - bei $1400, (hii bei inafanya ufikiri mara 2 kabla ya kununua; ni hela ndogo sana kulingana na jina hilo la gari), inawezekana ilipata ajali ndio inauzwa hivyo, wenzetu wako makini sana na uzima wa gari na 2 - imeenda km 120,000 hapa ni vema upate gari iliyoenda chini ya km 100,000 maana ikifikia 160,000 engine inakuwa imechoka, bora bodi ichoke utafunga mpira na kuziba kwa bati, ila sio engine (majanga). Bahati mbaya huku kwetu hatuna mitambo ya kupima uzima wa gari (engine), Ulaya na US wana kitu wanaita Emission Test; hii ni njia inayotumika kwa kutumia computer kupima uimara wa engine; kinachofanywa engine inawashwa na kuzungushwa mpaka engine rotation kubwa iwezekanavyo, na hivyo kutoa moshi unaochambuliwa na computer. Computer itatoa matokeo kwenye graph kuwa ama ni PASS au FAIL, kama ni FAIL basi lazima gari itengenezwe angalau iwe vizuri ili kuweza kuruhusiwa barabarani ( huku kwetu tunaita Road License ya kila mwaka)
Kitu kingine, ambacho huku kwetu hakuna ni Car History; hii inatoa maelezo yote ya gari tangu imetoka kiwandani; imeshakuwa na wamiliki wangapi, ajali ngapi na matengenezo yake kwa kiasi gani. Kwa kuwa hii hatuna huku kwetu basi tunanunua magari kwa gharama kubwa isiyohitajika plus ushuru.
Hata hivyo, bado sio sababu ya wewe kuacha kununua gari; wakati mwingine mara nyingi tu waweza kupata gari nzuri
Asante
 
Asante sana,pamoja sana....
je nikiiagiza kwa bei hyo huku nitaitoa bandarini kwa bei gani,mchanganuo wa bandarini cjaujua vzr
 
Back
Top Bottom