Msaada mwenye mawasiliano na NIC

Nduvajbn

New Member
Feb 11, 2018
2
0
Jamani msaada.
Nilijiunga na bima ya maisha ya Sh.3,000,000 na Shirika la Bima la Taifa (NIC) tangu mwaka 2012 kwa makubaliano ya kulipwa 20% kila baada ya miaka 3.

Lakini mpaka sasa ni miaka 8 sijapata chochote nimefuatilia ofisi za bima Sumbawanga lakini kila siku naambiwa subiri, nimewapigia simu makao makuu lakini simu yangu haipokelewi, nimetuma Email mara kadhaa lakini hakuna majibu yoyote.

Kwa anayejua namna nyingine ya kuwasiliana nao naomba anisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NIC ni visirani ....matapeli wakubwa tena wezi.
mimi nilikata bima ya maisha mwaka 1998 ya kiasi cha milion 2.5 na bima yangu iliiva tangu 2016.
Bima imeiva lakini kila nikifuatilia majibu ni utapeli tu mara nenda urudi baada mwezi mmoja mara mkurugenzi yupo Morogoro yaani ni wizi mtupu.
 
Umeisha tapeliwa, pole sana. Hao watu hawana tofauti na BAYPOT na FAIDIKA, walisha nichomesha mahindi kama kawaida yao. Waajiriwa wapya ni wahanga.
 
Nakuonea huruma,NIC ni wezi lakini tatizo si lao kuna watu wamefanya pale kama kisima cha kuchota fedha na huwa hazirudi kwa hiyo kulipwa utasota saaaaaaaanaaaa.Pole
 
Hao jamaa hawafai hesabu maumivu tu ila ukikomaa sana watakupa hata robo ya kukutuliza!
 
Kikubwa ni kwenda TIRA (Tanzania Insurance Regulaory Authority) maana wao ndiyo mamlaka ilipewa nguvu za kisheria kusimamia kampuni zote za bima nchini. Ni kama ilivyo TRCA kwa kampuni za mawasiliano. Nenda z=na ushahidi wote (vielelezo) vinavyoonesha wee ni mteja wa NIC na ulipaswa kulipa mwaka huo lakini hadi sasa bado unapigwa tarehe tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom