Msaada: Mwanangu hapendi kula

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Salaam wana HHM

Jamani mi nina mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 4 na miezi kama 8 hivi

Huyu mwanangu anaishi na mamake mkoa jirani na ninaoishi Mimi,kila Mara napata malalamiko toka kwa mamake kwamba mtoto hapendi kula.

Na hapo kwa mama mtoto pako vizuri tu kuhusu misomi ,yani balanced diet ipo ya kutosha ,ila mwanangu ndo hivyo hapendi kabisa kula

Afya yake haiko poa yani mwili ni mwembamba haswa yeye msoc wake anapenda chips tu,akipewa vyakula vingine vyenye lishe hali na akila basi kwa kujilazimisha.

Mimi ninapomtembelea ndo anakula kwa sababu namtisha ntampiga

Sasa naombeni ushauri nifanyaje huyu mtoto apende kula na anenepe na asiwe anamgomea mamake mida ya kula

Manake mamake hata kumpiga hampigi ili kumtisha aweze kula

Nipeni njia rahisi za kufanya ili huyu mtoto apende kula.

Asubuhi njema.
 
Hata mtoto wangu ilikuwa ngumu sana kula hasa ktk umri huo ijapo hakung`ang`ania chipsi. Sasa kwa vile mama amemzoesha chips, jaribu kumpa chipsi kidogo baada ya kila mlo kamili(baada ya balance diet). Hii fanya kwa kila mlo hata kama ni mara tatu kwa siku. Asipokula mlo kamili usimpe hiyo chipsi kidogo. Akizoea hivyo baadae labda mpe chipsi kidogo mara mbili na chakula kamili mara tatu. Utampa chipsi labda mchana na jioni. Akizoea hivyo baadae utampa chakula mara tatu kama kawaida na chipsi kilogo jioni tu. Akizoea hivyo utampa chipsi mara moja jioni labda kila baada ya siku mbili na baadae mtaendelea wenyewe kutokana na hali yenyewe.....
Kwa kweli chipsi ni mbaya sana ndugu yangu kwa kila mtu na hasa kwa umri wa mtoto. Watoto wengi siku hizi wamekuwa wanene na hiii inaathiri sana afya zao.
Kila raheli
Umesema misosi ipo, anapokula hata kdg apewe vyakula vyenye vitamin "B"
 
Achana na mambo ya kumpiga mtoto wa miaka 4. Kuhusu mtoto kukosa hamu ya kula ni vena ukaenda hospitali inayojielewa upewe ushauri na mtaalamu kulingana na hali ya mwanao. Lakini pia kama ulianza kumpa vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta(vya ku kaangwa) kama soda na chips, basi umesababisha tatizo wewe mwenyewe. Mwone daktari
 
Wangu pia ni hivyo. Nilienda hospital nijapewa multivitamin na sawa ya minyoo. Akaanza kuwa anakula ila sasa hali imekua tena kama mwanzo. Nafikiria sijui niende tena?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom