Msaada Mtoto wa Miezi Sita Anapata Shida Kupumua Usiku na Uzito Kutoongezeka

Uliweza kupata matibabu?
Nilipewa rufaa kuanzia wilayani, nikaenda Bugando then Muhimbili then rufaa ya India. Kumpeleka wakasema nilichelewa kugundua tatizo kwahiyo hawezi kufanyiwa operation kwan umri ulikuwa umeenda sana ilitakiwa afanyiwe akiwa na miezi 3. Nikarudi kwa neema ya Mungu mtoto anaendelea vizuri na kukua kwa taratibu lakini hasumbuki kama mwanzo.
 
Mkuu nakushauri mpeleke mtoto kwa specialist wa watoto.,
Private hospital...
Wachana na hospital za government.

Mtoto wangu alikuwa anaumwa, malaria ,
akapelekwa government hospital,
Wakati yupo kwenye foleni ya kumwona daktari akatapika sana,
Ikapelekea apelekwe kwa daktari haraka sn.

Doctor bila kumpima au kufanya uchunguzi wa kina ,
akaandika transfer kwenda hospital ya wilaya Mwananyamala hospital.

Kwa kweli walinijambisha sn Mwana nyamala hospital..

Napo kufika huko, manesi kumuangalia machoni mtoto,
wakasema hana damu ,,

Dah!! ilikuwa taharuki ya hali ya juu.,
Mbaya zaidi mtoto mishipa haionekani,

Baada ya purukushani za hapa na pale hatimae mishipa ikaonekana wakamuweka damu.,
Alilazwa kwa siku 3,
tukaruhusiwa kurudi nyumbani..

Nikapata wazo kwenda private hospital.
kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Sikuridhika na jinsi walivyompima hata kupata majibu ya kwamba mtoto wangu ana sickle cell.

Kufika private hospital walimpima Kila kitu,,
wakagunduwa hakuwa na sickle cell wala upuuzi wowote..
Hata damu aliyowekewa hakustahili kuwekewa.,
Alipaswa apewe syrup ya kuongeza damu na sio kuongeza blood ya mtu mwingine kwa drip.

Wakasema asitumie dawa zozote hadi miezi 3 nimrudishe tena hospital wampime tena.

Hawa madaktari wetu government hata sijuwi wapo pale kwa maslahi ya nani.
Wanaweza wakampa mtoto wako ugonjwa ambao wala hana,
Pengine ni tatizo dogo,wakalikuza na kuwa kubwa.

Namshukuru ALLAH,,
ALHAMDULILAH,,yupo ok hadi Sasa..

Nenda private hospital tafuta daktari wa watoto.
Kote ni wabovu uwe na bahati tu!

Nina mdogo'angu anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa na kuumwa sana upande mmoja wa mwili nimehangaika nae zaidi ya mwaka sasa zunguka hospital zote nzuri unazojua wewe pigwa mpaka MRI wenyewe wanadai ndo kipimo cha mwisho kwenye utambuzi wa maradhi lakini hola hawakuona tatizo dogo akawa analalamika bro nakufa huku najiona.

Huku kuongea ongea na watu vizuri nikaomba ushauri kwa jamaa na marafiki mmoja akaniambia nenda sehemu fulani hospital ya Wakorea ni mke na mume wanatibu kwa dawa za kutoka kwao nimempeleka dogo juzi jumanne wakampima kwa kipimo chao wakatoa majibu kwamba tatizo ni mishipa ya fahamu na pingili za shingo amepewa dawa na kuchoma sindano ananiambia ameanza kupata nafuu though ni gharama but kidogo nafarijika.

Tanzania ukipona au mgonjwa wako akipona mshukuru tu Mungu madaktari wanalipua sana kwenye kazi yao.
 
Kote ni wabovu uwe na bahati tu!

Nina mdogo'angu anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa na kuumwa sana upande mmoja wa mwili nimehangaika nae zaidi ya mwaka sasa zunguka hospital zote nzuri unazojua wewe pigwa mpaka MRI wenyewe wanadai ndo kipimo cha mwisho kwenye utambuzi wa maradhi lakini hola hawakuona tatizo dogo akawa analalamika bro nakufa huku najiona.

Huku kuongea ongea na watu vizuri nikaomba ushauri kwa jamaa na marafiki mmoja akaniambia nenda sehemu fulani hospital ya Wakorea ni mke na mume wanatibu kwa dawa za kutoka kwao nimempeleka dogo juzi jumanne wakampima kwa kipimo chao wakatoa majibu kwamba tatizo ni mishipa ya fahamu na pingili za shingo amepewa dawa na kuchoma sindano ananiambia ameanza kupata nafuu though ni gharama but kidogo nafarijika.

Tanzania ukipona au mgonjwa wako akipona mshukuru tu Mungu madaktari wanalipua sana kwenye kazi yao.
Kwakweli madaktari wanalipua sana sana sana cjui tatizo ni nn jmn ,natamani km cku waulizwe Huwa yanawakuta yapi ni madaktari Wachache mno hufanya kazi Yao Kwa moyo
 
Habarini wanajamvi

Nina mtoto wangu ana umri wa 6 month, ila baada ya mwezi mmoja mtoto alianza kua kama na mafua na kupata shida ya kupumua (anakua kama anakoroma akiwa anapumua) hasa wakativwa usiku japo hata mchana pia.

Tumeenda hospital kama mala 3 na kila wakimpima wanakuta hana tatizo na wananipa dawa za antibiotics tu na drops za kuweka puani ili mafua yasigande.

Sasa tangu wiki iliopita hali iliongezeka zaidi usiku anahangaika kulala sababu anapata shida kupumua na kijasho kinamtoka sana wakati hakuna joto, hata akiwa ananyonya lazima kijasho kimtoke hata kukiwa na baridi.

Madaktari na watu wenye ujuzi naomba mnisaidie tafadhari, sababu hii hali ya mtoto wangu inaninyima raha kabisa sababu akianza kushindwa kupumua hatulali hadi naskia uchungu.

Pia swala la mwisho ni tangu afikishe miezi 5 uzito wake ukawa ni kilo 6 na tangu hapi hadi muda huu anakaribia miezi 7 ila kila nikienda krinik uzito ni ule ule kg6 hauongezeki, tafadhari msaada wenu nifabye nini katika hili sababu mahali nilipo hakuna madaktari bingwa wa watoto.

Asanteni.
Muone daktari aliyeko karibu.

Pamoja utamuona dkt lakini mwanao anatakiwa kujengewa uwezo wa seli zake za mwili kukua na kukarabati moyo wake.

Kwa sababu ni mdogo muanzishie tiba ya stemcells ambayo itaondoa kilichoharibika na kujenga seli mpya ndani ya mwili wake.

Hata kama ni kweli au si kweli ana sickle cell itapigwa huko huko

Stemcell zinapatikana mlimani city dar es salaam
Piga namba hii kwa maelekezo zaid
0719794789
 
Sijui

Kwetu mtoto wa 2yrs alikuwa anapitia dalili hizo, ikqja bainika ni tonsils na nyama za pua
Miaka miwili sawa ,huyu miezi 6 hapa niziwa tu la mama ,na anaingia miezi 7 aanze kunywa maji na uji wakufa mtu mama ake aaze kuzurula na kidogo kuaza kuchachua ziwa ujuavyo hapa vidonda na mikwaruzo yoote imepona
 
Japo post ya 2022 jamani mtoto akiwa na shida mpeleke kwa Dr wa watoto sio kumpeleka kwa MD,natumaini mwanao alipata ufumbuzi yawezekana shida pumu, Nyama za pua au shida nyingine natumaini alishapata msaada kapona.mie sitakagi masikhara na afya ya mwanangu kuomba ushauri maana miluzi mingi ilimpoteza mbwa kila mtu atakuambia lake napambana na Dr wa watoto nikishindwa ndo ushauri labda kuna Dr best zaidi
 
Hakikisha hutumii feni mbele ya mtoto. Feni siyo nzuri kwa kifua
Feni sio shida wala haijawahi kuwa shida,shida mazingira wengi tunayo ishi chumba kama store 😁iwapo hakuna makokoro vumbi neat and clean fan salama kabisa fan
 
Back
Top Bottom