Ukiskia uchawi na kutaka kujikosesha baraka ktk maisha ndio hii. Umekutana na mtu amekupenda na kukueleza ukweli kwa kua unataka ndoa unakubali then ghafla unabadilika. Hivi ulikubalia nini at first place? Na kitabia hiki wanawake tunacho sana, kama hukujulishwa inaweza leta shida lakini ulijua kila kitu.
Mtoto ana umri gani? Naomba kaa nae ongea nae tu kistaarabu bila jazba aseme kwanini amebadilika gafla na kwa nini alikubali. Ikishindikana jaribu kumtishia kua ndoa itavunjika umuone amesimamia wapi. Ikishindikana kama umri wa mtoto unaruhusu mtafutie shule boarding awe anakuja likizo tu sababu namna hiyo ni hatari kwa mtoto Psychologically.
Alafu hizi one sided story isijekua amefikia uamuzi huo sababu nawe umebadilika na mmekua mnavurugana.