Msaada: Mpenzi wangu nahisi ni tapeli

Msaada: Mpenzi wangu nahisi ni tapeli

jaap

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2018
Posts
5,344
Reaction score
7,103
Nina mpenzi wangu ni bint mzuri tu,tatizo lake nimemchunguza nimegundua siyo mkweli muongo na mdokozi wavitu, kuna siku nilikuwanae ghetto niliamka asibuhi nikaenda kazini nikamuacha badae na yeye akaondoka, nilivyorudi gheto nikakuta pafyum yangu siiyoni, na siku nyingine niliamuacha gheto kurudi jion sabuni yangu ya unga sijaiyona na vitu vyote ivyo alivyo chukua nilikuwa nikiondoka asubuhi naviacha vipo! kwenye uongo:

Kila akiniomba msaada wa kipesa kununua kitu furani nikimpa sioni akinunua icho kitu alicho kuwa anakiitaji, aliniombaga hela yakununua kapeti nikweli alikuwa anashida ya kapeti, chakushangaza kapeti ajanunua na hela nimempa, na jingine kaniambia simu yake mbovu nimekuja kugundua simu ni nzima, na aliniomba ninunulie mashuka nikamwambia sawa naenda kukununulia nashangaa anataka nimtumie hela,

Mimi nikamwambia nipo dukani nanunua kabisa na nakuletea nikanunua nikampelekea kufika karibia na kazini kwake nika mpigia sim akawa apokea mwishoe akazima mpake kesho yake asubuhi, na nikimpigia hataki kupokea, kwa Mimi nimemgundua siyo mkweli anaomba hela yakutatua matatizo lakin siyoni akiyatatua, mfano ana mapungufu ya vitu nikimpa hela siyoni akivinunua ivyo vitu alivyo visema, na jingine nimegundua anatumia majina ya uongo,

Kwenye nyumba alipo panga kataja jina tofauti na aliloniambia, na kwenye line ya simu anatumia jina jingine na yote kayakubali.
 
😀😀Wanawake wa kiswazi taabu sana.

Kakubali dhiki zimtawale usimuache, mrekebishe taratibu mkuu. Ongea nae tu atakuwa ana matatizo mengi sana ya kiuchumi kama mtu anaondoka na mpaka sabuni ya unga.

Hana ajira na amepanga?au hajira yake haikidhi mahitaji.
 
Wanawake wa kiswazi taabu sana.
Kakubali dhiki zimtawale usimuache, mrekebishe taratibu mkuu. Ongea nae tu atakuwa ana matatizo mengi sana ya kiuchumi kama mtu anaondoka na mpaka sabuni ya unga.

Hana ajira na amepanga?au hajira yake haikidhi mahitaji.
Nishida wanakuwa waongo waongo kwa vidogo vidogo
 
kuwa naye makini mno,anaweza kukusababishia maafa

mademu wa sampuli hiyo hutumika na majambazi...na unaweza ukawa unakula dem wajambazi pia

mabinti wema wamejazana.Acha nae...

Samaki mkunje angali mbichi;huyo ameshakauka kama kaukau
 
Back
Top Bottom