Anayo hiyoMaradhi ya PID ndio maana akifanya mapenzi na wewe huwa anatokwa na Damu ukeni hiyo ni dalili ya ugonjwa wa PID aende Kutibiwa hospitali hiyo PID asipo pona zipo dawa za asili ataweza kutibiwa na kupona na kuweza kushika mimba kama akitaka.
UGONJWA WA VIUNGO VYA NDANI VYA UZAZI/PELVIC INFLAMATORY DISEASE (PID)
Utangulizi:
Mpenzi msomaji wa Health Media Tanzania leo tunaangalia magonjwa yanayoathiri viungo vya ndani vya uzazi kwa wanawake. Kitaalamu magonjwa haya yanajulikana kama Pelvic Inflammatory Disease kwa kifupi PID. PID kawaida au mara nyingi inawasumbua au kuwashambulia wanawake kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo nchi yetu Tanzania. Zaidi ya asilimia 60 ya wanawake wanaohudhuria kliniki za nje za magonjwa ya akina mama (outpatient) wenye matatizo ya ugumba yaani walioshindwa kupata mimba au watoto wanasumbuliwa na PID.
PID/Pelvic Inflammatory Diseae maana yake ni nini?
PID inamaanisha maambukizi (yaani infection) yanayoathiri viungo vya ndani vya uzazi vya mwanamke. Maambukizi haya yanajumuisha maambukizi katika kuta za ndani za tumbo la uzazi yanayojulikana kitaalamu kama “endometritis”, maambukizi katika milija ya kusafirishia mayai yajulikanayo kitaalamu kama “salpingitis”, maambukizi katika sehemu inayotoa mayai ya mwanamke yaani ovaries maambukizi haya kitaalamu yanaitwa “oophoritis” na mwisho maambukizi katika eneo lote la viungo vya uzazi yaana kitaalamu pelvic peritoneum na parametrium; maambukizi haya yanaitwa “Parametritis”. Kwa mantiki hiyo, maambukizi haya yote yanajumuishwa katika tafsiri ya neno moja ijulikanayo kama “Salpingoophoritis”. Hata hivyo, maambukizi madogo (mild infection) yanaitwa Pelvic Inflammatory Disease (PID).
AINA ZA PID
Kwa kawaida yapo makundi mawili ya aina za PID yanayojulikana kama “Primary” na “Secondary”.
Primary PID ni pale ugonjwa unapotokea mara ya kwanza kwenye viungo vyako vya uzazi. Mara nyingi inasababishwa na bakteria waitwao Kisonono kitaalamu aina ya Nesseria gonorrhea na Clamydia ambao bakteria hawa upanda kirahisi wakati mwanamke anapokuwa kwenye hedhi (menstruation) ambapo kunakuwa na damu ya kutosha na kuwapa bakteria hawa nafasi ya kukua vizuri. Kipindi cha hedhi bakteria hawa usambaa hadi kwenye kuta za tumbo la uzazi yaani kwenye “endometrium” na baadae kufika kwenye milija yaani “fallopian tubes” Kutokana na kuwepo kwa maji yanayotolewa kwenye ngozi ya fumbatio la viungo vya ndani yaani “peritoneum” usaidia bakteria hawa kutoka katika mijija (fallopian tubes) uweza kufika kwenye ovari kusababisha maambukizi katika ovari hizo yaani mayai ya kike. (oophoritis)
Maambukizi katika milija usababisha kukusanyika kwa maji (oedema) na usaha au maji maji meupe kama usaha. Hii hali usababisha maambukizi makali ambayo uweza kutengeneza jipu baada ya kusambaa katika fumbatio la viungo (peritoneum) ambapo jipu hili uitwa “pelvic abscess”. Hapa mgonjwa upata maumivu makali sana chini ya kitovu au kinene, upata homa kali sana, maumivu wakati wa kukojoa.
Kumbuka: Kisonono au gonorrhea unakipata kwa njia ya kujamiana.
Secondary PID ni pale ugonjwa unapotokea kama madhara yaliyotokana na ugonjwa wa kwanza au baada ya upasuaji katika viungo vya uzazi.
Madhara haya yanaweza kutokana na:
Upasuaji/operation ndogo ya kutoa mimba ambapo uishia kusababisha maambukizi yajulikanayo kama “post abortion sepsis”,
Maambukizi yatokanayo baada ya kujifungua yaani “postpartum sepsis”
Mimba iliyotungwa nje ya kizazi na kuharibika yaani “infected ectopic pregnancy”
Madhara ya kutoa uvimbe (fibroids) katika tumbo la uzazi yaani “myomectomy”
Upasuaji mkubwa wa kuondoa kizazi cha kike yaani “vaginal hysterectomy”
Kufunga kizazi yaani “tubal ligation”
Upasuaji katika milija wakati wa kuizibua yaani “tubal surgery”
Maambukizi katika madhara haya mara nyingi ni bakteria wanaotokana na choo/kinyesi. Bakteria hawa wanajumuisha E. Coli, Klebsiella, Salmonella, Proteus vulgaris, peptostreptococcus na streptococcus.
Utatambuaje kuwa una PID?
Dalili:
Kawaida utajisikia maumivu chini ya kitovu yaani kitaalamu lower abdominal pain.
Homa kupanda
Mapigo ya moyo kwenda mbio
Kuvimba tumbo
Kutokwa na maji machafu ukeni na yanatoa harufu mbaya na pengine kutokwa na damu ukeni yaani “vaginal bleending”.
Ushauri: Ukiona dalili hizi nenda kituo cha afya ukamuone daktari ili
aweze kukupatia tiba sahihi kwani PID inasababisha ugumba usipotibiwa vizuri na kupona kabisha.
Matibabu:
Kawaida matibabu yanategemea na ukubwa wa tatizo. Ukubwa wa tatizo umegawanywa katika makundi makuu matatu:
Acute PID
Mild Acute PID
Chronic PID
Kundi la kwanza na la pili yanatibiwa kwa kupewa dawa/tiba na mtaalamu wa afya hususan daktari.
Kundi la tatu yaani Chronic PID mara nyingi tiba yake ni dawa za kupunguza maumivu na pia kupata
ushauri wa daktari. Hakuna dawa unayoweza kupewa ili tatizo hili liondoke au liishe badala yake unatuliziwa maumivu tu.
Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa basi upasuaji (surgical intervention) unaweza kutumika kama njia ya tiba.
Madhara ya PID
PID isipotibiwa vizuri na kupona inaweza kuathiri afya ya mwanamke kimwili, kijamii na kisaikolojia.
Mgonjwa anaweza kuishia na kupata ugonjwa sugu yaani “chronic PID” ambayo uweza kumsababishia maumivu makali
wakati wa kujamiana na pia kupata matatizo ya mzunguko wa hedhi.
Na pia inaweza kusababisha jibu na pia maambukizi katika fumbatio la viungo vya ndani yaani “severe peritonitis”
ambayo ni hatari kwa maisha. Pia inaweza kuishia kutengeneza uvimbe katika milija na ovari yaani “Tubal Ovarian Masses TOM”.
Hii inaweza kupelekea kupata ugumba wa muda yaani “sub fertility” au ugumba wa kudumu yaani “infertility”.
Haya madhara umsababishia mwanamke kuathirika kijamii na kisaikolojia na pia umletea msongo wa mawazo.
Talaka, kutengana na hata kujiua (suicide ) ni matokeo ya kijamii na kisaikolojia ya PID.
Hitimisho:
PID ni sababu kubwa ya kusababisha madhara kwa wanawake.
Inasababisha madhara si tu kwa wanawake na pia kwa jamii nzima. Ina madhara kimwili, kijamii na kisaikolojia.