sasa mkuu hapo huna ujanja maana hata nkikutajia browser nyengine still utakwama maana utaoidownload vipi? hapo unahitaji udownload ucweb au opera nyengine (4.4 recomended)
jaribu kufanya hivi
1. connect simu na pc uangalie kama ina mass storage kama inayo download opera au ucweb kwenye pc halafu yahamishie kwenye simu, kujua kama ina mass storage ukichomeka simu kwa pc icon ya simu itatokea kwenye mycomputer na ukiiclick utaweza browse mafile ya simu.
2. ikishindikana hapo juu inabidi ukomae na browser ya simu ifanye kazi, sijawah iona hio simu ila ngoja nikutengenezee theory itakayokusaidia. opera inatumia access point ya internet mara nyingi na browser ya simu inatumia mtindo wa kizamani wa wap/web sasa unachotakiwa ni kutafuta wap setting uzieke kama mtandao wako unavyotaka.
3.njia ya tatu ni kuitrick opera isijue kua file unalodownload ni la jar na hii itabidi mtu aku uploadie file la jar lakini arename extension kuwa file jengine mfano opera.mp3 halafu ukishadownload unarename kwenda opera.jar then una install