Msaada: Mke wangu mvivu kupindukia!

Kama una ndugu au marafiki wenye wake wachakalikaji jaribu kumuweka karibu nao, ama kwa kuwatembelea au kwa kuwaarika nyumbani, wapo watu bila kuona Fulani anafanya nini ni wazito kufanya. Jitahidi umweleweshe kazi/biashara hatufanyi ili tupate pesa bali inaongeza thamani ya utu wetu na kuikomaza akili katika kufikiri.
 


daaah natamani ungekuwa mume wangu, eti unamlipa mshahara? mmmmmhhhh kuna watu wanabahati jamani lkn hawana shukurani kwa Mungu..
sis wengine ukizubaa mume anaweza akakaa hata mwaka hajatoa hela ya chakula, ada nk..
tunahangaika kusoma unamuomba mume akusaidie ada walau kidogo anakupiga tarehe hadi unamaliza masters umejilipia mwenyewe!!!!!!!eti unalipiwa kila kitu na vitabu umenunuliwa halafu unaacha shule? khaaaaaa ndio nasikia leo....kiruuuuu
unapewa mtaji unachezea biashara? heeeee!!!!!!!!!!!!halafu eti graduate?....yeleuwiiiiiii,
 
Huyo anabweteka kwa kuwa pesa ipo na anajua akikaa home au afanye kazi pesa zipo tuu, cha kufanya mtafutie kazi then mnyime pesa ili ajifunze na komaa na msimamo huo kwa wazazi wako ili wasimkingie kifua, ukivuta brother watu watajipigia tuu na watoto watateseka kwa kuwa mama yao hajishushughulishi. Nachukia sana mijitu ya hivyo yaani inapenda maisha ya ubweeeeeteeeeeeeee..... wanawake amkeni bana mbona maisha yamechange kitambo... mkisemwa mnang'ang'ania haki sawa.... Piga kazi maisha mchaka mchaka.
 
Unafuga matatizo halafu unaomba ushauri


Kata kumpa hela, na hata akienda kusema usimpe

Hakikisha ndani kuna chakula na yeye usimpe hata 500 ya kusuka twende kilioni

Hata vocha usimnunulie

Akikaa hivyo miezi 3 mingi atatafuta cha kufanya

Tena akimpa mtaji mpe 20,000 tu mwambie apike vitumbua

She needs to learn the hard way


Asipojifunza oa mke wa pili
 
Nilikuwa nishamchukia huyo mama baada ya kusoma post. Lakh.nh. we bwana Mungo Park umenibadili mawazo sana. Nadhani uko sahii. We should give that woman some benefit of doubt. That dude afanye kama ulivosema.
 
Last edited by a moderator:
Mpe talaka arudi kwao alafu oa Mwingine.
 

hahahaaaa!!kashika pabaya aisee
mama mkwe ndio rafiki yake,kazi ipo
labda umweleze mama jinsi unavyokereka
kwa kua ni mtu wake wa karibu na ni mzazi
ajaribu kuongea nae,dunia ya leo sio ya
mwanamke kubweteka,ukitoweka ghafla
ataishije na watoto,kweli kwny miti hapana wajenzi!!
 
Hebu mdadisi aliwezaje kumfanya mama yako mzazi awe rafiki yake mkuu halafu uje utupe feedback? Back to the topic. Hivi wewe ndugu ni nini hasa kilichokufanya ukaamua kuoa? Ni sura, elimu, mautamu ya ngono zembe za kabla ya ndoa, au matarajio ya kazi ya mke?
 
Tatizo utakuwa wewe, yaani huyo mwanamke angejua angekukimbia sababu hujitambui
 


100% support to commanche's post. read that over n over, brother!
 
Kaka Ujaeleza Kwamba Vp Na Kitandan Napo Mvivu Au Mana Ndo Kwa Umuhimu Ili Nikushauri Vizurioto wa 2. Nlimuoa mwanamke aliyekuwa kamaliza degree ambaye alikuwa home tu at the time anatafuta ajira. Toka nimuoe hajawahi kufanya kazi yoyote ile yaani Goalkeeper mpaka leo na kutafuta kazi alisha acha. Mpaka leo hii mke wangu hajabadilika. Namlipa mshahara mwisho wa mwezi ambao ni sawa na kama 10k per day yaani (300k). Kila ninapojaribu kumtafutia kazi anafanya kidogo tu anaacha. Huwezi amini hata umlazimishe vipi ajishughulishe mzito ile mbaya. Mi ni mfanyabiashara(Magari Makubwa) nimemuanzishia vimiradi through the years vyote kala mtaji. Kuna kipindi alijaribu kusoma masters ya bussiness administration nkamlipia ada, nunua vitabu vyote alafu yeye akaamua kuacha baada ya mwezi tu Eti kuamka alfajiri hawezi. Nkaja nkamuomba basi asome chuo ambacho atakuwa anaingia mchana nacho alishindwa.

Tatizo rafiki yake mkubwa ni mama yangu mzazi hivo kuna kipindi nlikata mshahara wake ili kumlazimisha afanye kazi aki
 

Kama ni kweli uliyoandika pole sana. Mkalishe chini, mwanamme aliyekamilika huwa siyo mtu wa kulalamikia mwanamke. Angekuwa amekukimbia akakuachia watoto hapo sawa. Mwanamme riajli huwa anachukua hatua za kutatua tatizo kwa busara na amani. Kwenye jukwaa hili ukifuata sana ushauri nina wasiwasi wanaweza wakaja wengine wakakunyonyesha kasa. Chukua hatua!
 

Mie mwenyewe nimesikitika aisee kuna watu wanatamani wapate hata mume

wa kumuachia hata mia ya 5 ya mboga haapati......huyo siku akipewa talaka aje

alalamike!!!!!!!7 years inaonekana na yeye hii tabia ameilea yeye......azungumze nae tu
 
Ndo maana staki mke wangu awe 'that close' na mama yangu, the point is amuheshimu tu but 'ushosti' hell no. . .coz najua kuna maamuzi ntashindwa kufanya kisa mke wangu anashauriana na mama angu.
 
Ila mkuu slave inaelekea hauko strict. . .unajua a bit of strictness kwa mwanaume sometimes inahitajika. . .
1. Alipoacha shule kisa kuamka asubuhi..
2. Matumizi mabovu ya pesa (hapa yani tena kwa siye mangi ndo nakutoa na ngeu kidogo)pesa haziokotwi ndugu, zinatafutwa.
3. Kutokua serious kwenye biashara. . .aisee. . Muke ya mangi hapa angechezea kichapo tu hapa.
Nakushauri ndugu yangu, as you know our women wanapoteza muda kwenye vitu ambavyo vina non financial returns,
1. Jaribu kuangalia vitu anavyopenda kuvifanya na havina manufaa yeyote kwako na kwa familia yako halafu umkataze.
2. Kaa chini umueleze namna ambavyo hupendi uvivu wake na hatua ambazo unaweza kuzichukua.
3.Mama yako naye ana role kubwa pia kwenye hili, kaa naye umueleze kuhusu mkeo halafu uone na yeye kama ana mtazamo sawa na wewe.
4.Have a last shot, mfungulie biashara ambayo hatakua anaisimamia directly, waweza tafuta mtu kwanza, either ndugu yako wa karibu or rafiki mwenye uzoefu wa muda mrefu kwenye biashara awe anamsaidia in the first few months huku akiwa ana catch up taratibu.
5. Haya yote yakikataa or ukiona hamna muelekeo (ila sishauri saaana) mpe talaka moja aende nyumbani kwao akatafakari, hii ina influence kubwa kisaikolojia who knows akirudi atakua tofauti.(by the way naomba kujua amesomea nini, u just said a degree)
All the best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…