Msaada: Mke wangu ameanza ushirikina

Ulichokileta kinadhalilisha Avatar yako...., inaonekana uliiweka tu hiyo avatar ila huendani nayo
 
nkadhani umekutana na power bank inapumua!! ni vizuri kushika mtoto ukiwa msafi, mihangaiko ya siku nzima tena kama unaishi Dar na huu mjoto hukawii kumwambukiza mtoto kikwapa
 
Usimfikirie vibaya bila uthibitisho... Ukute hivyo ndivyo alivyofundishwa kwao. Mda mwingine mtu ukitoka kazini unakua na jasho, vumbi na sometimes manukato mbalimbali... Atakua anahofia mtoto kupata mafua.
Ila hili ilibidi akwambie! Jaribu kuongea nae pia. Kama ni mtoto wa kwanza wengi wanahangaika na ushauri wa watu jinsi ya kulea.
 
Kama mama watoto amesema hivyo na unaweza, basi Fanya.

Mtu akitoka kwenye mihangaiko, akarudi nyumbani, huwa ni vyema kunawa mikono kwanza ili umshike mwanao.

Kuoga ni bora zaidi. Lakini kuoga bila kubadili nguo ni yale yale. Akina baba wengi huwa tuna nguo za nyumbani na nguo za kutokea.
 

Nasisi tuzae wetu basi
 
Njoo ufanyiwe maombi
Hakuna mchawi anayekatiza mbele ya Yesu.
 
Ivi kumbe ktk ndoa ndo kuna mengi hivi?
 
Fanya kumsikiliza maana nyie ni mwili mmoja na usipo msikiliza utakuwa hujamtendea haki.
 
Tekeleza hadi atakapukuwa anaanza kutembea atalegeza tu.Kwani wanawake wengi wanaamini usalama wa mtoto kiusafi na kiroho
 
Sio ushirikina mkuu mambo ya mila hayo, huwa wanasema mwanaume anaweza toka kuchepuka huko na kimada then akirudi nyumbani anakuja kumshika mtoto sasa hiyo wanasema sio nzuri kwa afya ya mtoto ndio maana wife anakwambia ukaoge kwanza kabla ya kumshika mtoto.
 

Ni wewe au kuna mtu kakuandikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…