Habari wakuu,
Bila kupoteza muda naombeni ushauri haraka sana kabla sijafanya maamuzi ya mwisho, ni hivi mimi nimekua kwenye uchumba na mrembo wangu kipenzi kwa miaka mitatu na mpenda na ananipenda in short tunapendana sana na tunaaminiana sana.
Mwanzoni wa penzi letu tuli enjoy sana ila mwenzangu alihisi kuna kitu namnyima maybe na kula ujana kwanza ndo maana simchangamkii sana kumbe na mimi nilikua najipanga kwa majukumu si unajua tena swala la kuchagua wa kuishi na kufa nae sio dogo sasa hakufurahishwa ila nilikua na lengo jema, nilikua nafanya maamuzi sahihi.
Mwaka wa pili nae akaanza vimbwanga, ndipo mihasira ikanijia kwa ghafla nikajiuliza kwanini hivi? Kwanini tusile mibata na kufurahia ujana kabla uzee haujaingia kama tutajaliwa pumzi na maulana? Matokeo yake penzi linakua chungu wala sijamfanyia usaliti au chochote kibaya?
Nikaja kubaini bwana huyu bibie ni egocentric/mbinafsi/mtu anayejipenda yeye tuu pasipo kujali hisia zangu.
Dah! Niliumia sana ila kwa kua nishampenda na kumkabidhi moyo wangu sikua na jinsi zaidi ya kumvumilia tuu mambo yasonge coz tuna katoto kamoja.
Nikasema nikiachana naye mimi nitakua mbinafsi pia sababu sitamjali huyu malaika coz bado ni mdogo ana mwaka mmoja na nusu, malezi ya bila baba na mama yake halisi sio mazuri kwa kweli.
So nikavaa roho yangu ya ukwere japo ni maisha ya kitanzi sina jinsi wala sina mpango wa kando “mchepuko” wala mapombe huko japo nijifariji. Nitakomaa na msalaba wangu mpaka mwisho.
Nilichokipanga ni kumnyoosha huyu mwanamke kwa njia za kitaalamu maana hakuna mfupa uliowahi kunishinda na ukinishinda uanaume wangu utakua umeshuka kwa asilimia 80%.
Hebu wakuu nisaidie namna ya kuondoa ubinafsi/kujipendelea zaidi toka kwenye nafsi ya huyu kiumbe. Maana lengo la kuwa pamoja ni kuliwazana, kusaidiana na kuendeleza lile jukumu la maulana “zaeni muongezeke muijaze dunia” Sisi ni vijana bado nina miaka 25 na yeye 23, nina degree na yeye diploma, nimemuoa mwaka jana 21 January 2017.
NB: Hii ni jambo la kweli maishani mwangu. Sisi ni wakristu tunamuamini Mungu kabisa wala hakuna influency ya shetani wala wasiotupenda, ni sisi wenyewe yani.
Nitashukuru kwa chochote.