Mshahara wake sidhani kama unavuka net ya 3.5m ila kwa mtu ambaye anaingia huko vyuoni sio tu suala la mshahara, anabidi aangalie uwezekano wa kukua professionalyl na academically. Kwa uelewa wangu mdogo PhD holder ana majukumu matatu akiajiriwa chuoni ambayo ni research, consultancy, teaching.
Ajiulize kati ya huko Afrika ya Kusini na Tanzania
- Ni wapi pana fursa kubwa ya kufanya tafiti (kwamba atapata research funds, na connections kwenye field yake kiurahisi) ?
- Ni wapi kuna uwezekano wa kupata consultancy projects kubwa na kujijenga jina lake ?
- Ni wapi pana uwezekano wa kupata support pale anapotaka kufanya machapisho (publishing) ya matokeo ya tafiti zake.
- Ni wapi pana masharti rahisi zaidi kupanda ngazi kutoka pale alipoajiriwa.
- Ni wapi kuna teaching workload yenye unafuu ili aweze kufanya mambo ya personal growth.
Maisha ya academics yanahitaji ujanja sana wa maisha kutegemea mshahara peke yake kama kigezo cha wapi afanye kazi inaweza kuwa si jambo sahihi.