mrdream
Senior Member
- Mar 23, 2014
- 122
- 245
Wakuu naomba msaada wenu wa ufafanuzi wa sheria. Nililipa mahari mwaka 2012. Tukapata watoto mapacha mwaka 2014. Tulifunga ndoa ya kiserikali mwaka 2015. Sote ni watumishi wa umma. Tunafanya kazi mikoa tofauti. Mwaka 2016 alikataa kuhamia ninapofanyia kazi tukaingia kwenye mgogoro akabaki na watoto. Mwaka 2018 ameamua kuwabatiza bila kunishirikisha na amegoma kutuma copy za vyeti vya kuzaliwa na copy za vyeti vya ubatizo. Nimejaribu kuhusisha wazee wake kwa hili wapo pamoja na binti yao. Hakuna ushirikiano kabisa. Nifanyeje. Watoto wana miaka mitano sasa. Je nitawapata baada ya kutimiza miaka saba? Je majina waliyowabatiza itakuwaje?