Msaada: Matumizi ya umeme

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,357
6,422
Waungwana,

Naomba msaada wa kiufundi.

Najikuta natumia umeme mwingi wa units 8/24 hrs. Matumizi yangu ni taa za save energy na friji ya kawaida moja tu. Nadhani kuna tatizo hapa maana unit 8 kwa siku ni nyingi.

Tafadhali naomba mawazo tatizo linaweza kuwa wapi
 
Isije ikawa una jirani kajiunganishia umeme kinyemela. Unaweza kufanya jaribio la kuzima kila kitu au zima main switch yako kwa muda fulani (1-2 hrs) halafu uangalie Kama Units zitatafunwa ndani ya kipindi hicho.
 
Waungwana naomba msaada wa kiufundi. Najikuta natumia umeme mwingi wa units 8/24 hrs. Matumizi yangu ni taa za save energy na friji ya kawaida moja tu. Nadhani kuna tatizo hapa maana unit 8 kwa siku ni nyingi.
Tafadhali naomna mawazo tatizo linaweza kuwa wapi

Wiring ya kizamani mita za kisasa. Unatumia mita za aina gani. Mkuu upo kwenye fremu. hena? (si ndio)
 
Uko wapi wewe? Kuna sababu nyingi, toa tu hiyo ni riziki ya fundi usijeambiwa kitu ukajaribu na kuunguza nyumba.
 
Sema ulipo usaidiwe, uwe tayari kulipia, kuna tatizo la kiufundi hapo linarekebishika.
 
Fanya kwanza hiyo test rahisi uliyoshauriwa hapo juu kabla hata ya kumwita fundi.
~zima main switch halafu record unit zilizopo.
~baada ya masaa 2 au 3 record unit tena
~linganisha units, kama zimepungua mtafute fundi.
~kama ziko vilevile kuna mawili kwamba fridge yako inatumia umeme mwingi au meter inahitaji kuangaliwa na tanesco.

Je, fridge yako ina watts ngapi?
 
Hili ndio jibu sahihi
 
Back
Top Bottom