Mkuu mie hii Hali ilianza nitokea 2010 mpaka saivi ninayo.
Nilikuwa nakaa Sana nasoma afu ulaji ni wali Sana.
Sema kweli ukilainisha choo inatoka kawaida.
Sema uvimbe huwa unatoka nje unapojikaza wakati wa haja.
Ukiwa unasafisha una feel sema unarudi.
Yaani kama mazoezi nilipitia jakata piga Sana tizi Ila hakuna kupungua..
Pokea ushauri na uwe serious kuufanyia kazi utapona
Kwa maisha ya kawaida ya watu wengi huwa na milo mitatu kwa siku katika hiyo milo mitatu hakikisha mlo mmoja unakuwa wa matunda pekee
Utachagua mwenyewe kama ni wa asubuhi, mchana au jioni na matunda hayo yawe mchanganyiko mfano Papai, chungwa, tikiti, ...embe, tango parachichi,carrot Nk
Hakikisha unakuwa Rafiki mzuri wa Maji
Yaani hakikisha angalau isipite siku hujanywa walau lita Mbili au zaidi za maji
Japokuwa utaenda haja ndogo mara kwa mara lakini ni Afadhali usumbuke kwenda haja ndogo kuliko upasuliwe na kuchomekwa mipira na plastics
Punguza vyakula vya wanga kama wali mfululizo....punguza sana au acha kabisa kunywa uji wa lishe au wa ulezi kwa maana una tabia ya kukausha choo sana ....
Ili kuthibitisha hili kama umewahi kuona kinyesi cha watoto wadogo wanaokunywa uji wa lishe mfululizo...
Kula vyakula vya mboga kama bamia ...nyanya chungu (ngogwe)...Biringany kwa wingi...kwa maana vina nyuzi nyuzi zinazosaidia kusafisha utumbo mpana na kulainisha choo...
Kama ni mlaji wa Machungwa basi unapokula chungwa usiishie kunyonya maji tu ka kutupa yale manyuzi nyuzi hapo utakuwa unapoteza kitu kikubwa sana..kula na nyama na nyuzi zote za ndani zina faida sana sana
Tatizo lako kwa 90% limechangiwa na ulaji Mbovu usio na mpangilio, pamoja na
Kutokunywa maji kwa wingi...
Zingatia niliyoandika hapa utaona mabadiliko...na utapona.
Ukipuuza shauri yako.